Jumatano, Julai 13, 2016

HUWEZI KUMZUIA KUKU KUTAGA



Ni ukweli usiopingika kuwa huwezi kumzuia kuku jike kutaga mpaka hapo utakapo mchinja.Lakini akiwa bado yuko hai hakuna namna utaweza kumzuia kuku huyu  kutaga.

Wengi yawezekana hawaamini hili kwa kwa kuwa hawajawahi kufuga kuku lakini kwa wale waliobahatika kufuga kuku hilo jambo wanaliewa.

Nilpokuwa mtoto nilikuwa mtundu na mdadisi japo si sana.Niliwahi kufanya majaribio kadhaa kumzuia kuku asitage nikaambulia ola maana kuku huwezi mzuia kutaga kivyovyote.Mama yangu alikuwa mjasiriamali wa kijijini kwa wakati huo kupitia ufugaji wa kuku.

Wakati kuku akiwa anataka kutaga huwa anahangaika ,anazunguka zunguka kupata mazingira mazuri ya kutagia na mara nyingi hupendelea kutagia bandani.Sasa fanya kama unafunga banda kwa kufuri ili asitage ,kuku huyu utakuta katagia kwenye nyumba ya kulala watu .

Kuku huyu huyu anapoona nyumba na mazingira ya karibu siyo wezeshi kwa yeye kutaga ,hukimbilia nyumba ya jirani na utasikia majirani wazuri wanakwambia "Aise fulani kuku wenu huwa anatagia kwetu na tayari ameshataga mayai kadhaa".

Kuku huyu huyu anapoona mazingira ya jirani yamemgomea yeye kutaga yai lake zuri linalomsumbua ,huenda kichakani na kutaga huko bila kujali chochote kama vile mayai yake kuliwa na wanyama na hata yeye mwenyewe kuliwa(ana roho ngumu).Huchukua maamuzi ya kijasiri kupata yai lake moja tu .

Kuku huyu nataka nimfananishe na binadamu ambaye ameona fursa ,ana ujuzi na mambo kedekede lakini utamsikia akisema mazingira haya siwezi kufanya chochote huku akitoa sababu za kushindwa kutekeleza jambo hilo(iga kuku mtetea).

Watu wamekuwa wanataja sababu kedekede ya kwanini wamedhindwa kufanikisha jambo fulani lakini ukweli ni kwamba hujafikiri kwa kina namna ya kulifanikisha(rejea kwa kuku mtetea).

Fursa uiyonayo sasa itazaa makubwa(mayai) na sasa kama utashindwa kutekeleza na kuingia moja kwa moja kwenye utendaji maisha yako yataendelea kuwa yale yale na utakuwa wimbo wako wa kila siku.

Umekuwa mtu wa tahadhari nyingi katika kujaribu kila mzaingira na kuku amekushinda akili maana kuku huenda mpaka vichakani anapoona mazingira ya nyumbani yameshindikani na kule kichakani hafikirii kingine lakini hufiikiria yai lake .

Naomba mayai yetu(fursa) tusizipoteze ati kwa sababu ya mazingira
(watu,vikwazo,mitaji n.k).

Narudia kusema Huwezi kumzuia kuku kutaga labda umchinje .

Joas(Jyb)







Maoni 2 :

  1. Ni hazuiliki kuku hazuiliki

    JibuFuta
  2. akuna mtu anahe weza kuzuulia kuku kutaga kamwe au hivi una weza kuuzuwia mbuzi kuzaha au nipeni jibu kwa sasa please

    JibuFuta