Alhamisi, Julai 28, 2016

"SIZITAKI MBICHI HIZI "




Wengi tunakumbuka shairi la sungura ambalo tulipitia wakati tunasoma shule ya msingi .Unaweza kuwa hukumbuki vizuri lakini usijali nitakukumbusha .

Mwandishi  wa shairi hilo alieleza jinsi ambavyo sungura alikuwa ameyatamani matunda na akaanza safari ya kufikia matunda yale .Akiwa katika jitihada za kuyafikia  akawa amechoka na akatoa kisingizio kuwa ndizi zile zilikuwa mbichi na sasa alikuwa hana haja ya kuzifikia.

Mshairi katika shairi hilo anasema kuwa Siyo kwamba ndizi zilikuwa mbichi lakini ukweli ni kwamba ndizi zile zilikuwa mbivu lakini Sungura alishindwa kuweka jitihada na bidii kufikia matunda yale .Mwandishi wa shairi hilo katika baadhii ya beti anasema :

"Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wake akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia."

Mafanikio yako ni ndizi mbivu ambazo ukizipata utafurahi maana mafanikio ni matamu .Kupata mafanikio siyo lele Mama inahitaji kujitoa mhanga na kujaribu bila kuchoka .Hakuna mtu adiyetaka kufanikiwa isipokuwa tunaogopa kulipa gharama(Paying the price ) na hata sungura alihitaji kupata ndizi zile mbivu lakini alizikosa kwa sababu aliogopa kulipa gharama .

Kuna mahali utafika na hakuna mtu atayekwambia kuwa sasa unakaribia kufanikiwa na kwa kuwa hakuna mtu atakayekwambia kuwa sasa unakaribia kufanikiwa unaweza kuacha kufanya biidii na hivyo ukaishia njiani .Haina haja ya kujichoisha kama unajua kuwa utaishia njiani .Safari uliyoanza unahitaji kuimaliza .Mwanzishaji wa jambo ndiye anapaswa kumaliza jambo .

Wakati sindano inataka inatolewa mwilini huwa ndipo maaumivu yanazidi kuliko pale inapokuwa inaingia mwilini.Wakati unakaribia kuifikia ndoto zako maumivu yatazidi na utahisi kuacha na utataja sababu kama za sungura na maisha yatakuwa yamekushinda na watu watakucheka ....Kwanini uchekwe??? kwanini ukate tamaa??? kwanini

Usiache kufuata ndoto yako ,wewe ni mshindi zaidi ya mshindi ,una kila kitu cha kukufanya ushinde , huyo anayekwambia huwezi siye aliyekuumba na hata hajui nguvu na uwezo ulioko ndani yako .Shida hujajua wewe ni nani na unapaswa kuwa wapi wa wakati gani na kwanini ulizaliwa wewe na si mwingine ....

Mwandishi wa shairi la sitaki mbichi hizi anamaliza katika ubeti wa mwisho kwa kusema yafuatayo:


"Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi."

Joas(Jyb) 0753836463







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni