Jumanne, Julai 26, 2016

FANYA KAZI KWA AJILI YA VIZAZI NA VIZAZI


Wakati nakaribia kumaliza Elimu fulani mahali fulani nilikuwa na kawaida ya kukaa na marafiki tukijiuliza nini kitafuata baada ya kumaliza na kuingia mtaani.

Wengi waliamini kuwa baada ya kumaliza wangepata kazi nzuri ambayo ingewalipa pesa nzuri na hatimaye kupata mambo waliyodhani kuwa vipaumbele kama vile kupata ndoa nzuri , gari ,nyumba ,mavazi,shule nzuri kwa  watoto wao n,k.

Swala ambalo wengi tumejisahahu ni kwamba tumekuwa tukifanya kazi kwa ajili ya maisha yetu binafsi bila kuangalia kizazi tunachotengeneza kitaishije.

Je unataka mtoto wako akimaliza abebe bahasha kama wewe ulivyofanya wakati umekuwa kazini miaka 20+ au hata 15?

Je unataka baada ya kustaafu ukaombe shule ya kufundisha badala ya kwenda kwenye kampuni yako ?

Ndugu zangu ipo haja ya kugeuza fikra zetu za kufanya mambo kwa ajili ya mambo ya muda tu bila kuangalia maisha baada ya kuzeeka,kustaafu ,kuachishwa kazi n.k.

Mwandishi mmoja anasema kuwa binadamu ni kama digidigi au simba .Anaeleza kuwa wakati simba anamfukuzia digidigi mara nyingi digidigi hushinda mbio hizo ili asiwe kitoweo cha simba .Lakini simba huwa hajiumizi sana kukimbia maana anajua atapata kitoweo kingine.Swali ni je kama digidigi akisimama atapona?.Jibu ni hapana.

Mwandishi  huyo anafafanua mfano huo kuwa :

  • Kama ikitokea ukaachishwa kazi leo maisha yako yakayumba basi wewe ni digidigi
  • Kama ukistaafu leo maisha yako na familia yako ikayumba wewe ni digidigi
  • Kama ukaumwa leo usirudi kazini maisha yako yakayumba basi wewe ni digidigi ambaye mara asimamapo tu wakati anafukuzwa na simba huwa kitoweo

Wewe ni shahidi hapo mtaani kwako:

  • Yule ndugu aliyestaafu unajua maisha yake yalivomagumu kama vile hakuwa kufanya kazi
  • Yule ndugu alivyopata matatizo na akashindwa kurudi kazini unajua maisha yake yalivyo ya shida 

FANYA KAZI KWA AJILI YA VIZAZI NA VIZAZI SIYO TUMBO LAKO TU.
USIPOKUWAMAKINI KESHO UTACHEKWA

Joas(Jyb)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni