THAMANI YANGU


NAMNA YA KUISHI  MAISHA  YENYE  MAANA

Utangulizi .

Watu wengi hudhani kuwa maisha ni uwezo wa kupata mahitaji yake binafsi (Kupata
gari,mke au mume mzuri ,fedha,kula vizuri   n.k)

Wapo watu wanaoamini kuwa maisha ni kusoma ,kufaulu na baadae kuja kuajiriwa na kuwa mtu mkubwa sana na mtu mwenye heshima mtaani .

Nilivyokuwa chuo kikuu mahali fulani niliwasikia vijana wakisema kuwa maisha yatakuwa yamekamilika pale watakavyomaliza na kupata pesa nyingi zitakazowawezesha kupata kila wanachokitaka (mke au mume mzuri ,gari ,starehe n,k).

Jamii huamini mtu asiye na fedha ,cheo ,umaarufu , shule huyo hana maisha  na mtu huyu hudharaaulika na yeye mwenyewe hufika mahali anakata tamaa na kuona kama amezaliwa wa bahati mbaya na hana maisha .

Ukweli ni kuwa kuwa na fedha ,vyeo na kila kitu hakuwezi kusababisha kuwa na maisha yenye maana.

Maisha yenye maana ni nini basi?????
 je ni kupata mke/mume  mzuri na kuwalingishia wenzako????
je ni kupata elimu nzuri ????
je ni kupata mali na kila kitu ????

maisha yenye maana ni haya hapa

Kujua Kusudi la kuja HAPA duniani .hujalijua kusudi hujaanza kuishi

kanuni ya kuishi maishi yenye maana ni hii hapa

Thamani yako(your values)+Uwezo wako(your core strength)+Kiu yako(Your Passion)+ huduma yako(your service )=Kusudi lako=maisha yenye maana

Ili uishi maisha yenye maana lazima ufuate kanuni hiyo vinginevyo maisha yako hayataleta maana yoyote hapa duiani haijalishi utakuwa na vingapi vinaavyoonekana .




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni