Jumamosi, Julai 23, 2016

" USIPOTELEE MWISHO" ~JOAS Yunus






Emanuel Mgogo mwimbaji wa nyimbo za Injili katika moja ya wimbo ulio katika albamu yake mpya anasema " siku moja alikuwa anasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa basi na wakati wanakaribia kufika mwisho ,ghafla ajali ikatokea na watu wengi walipoteza maisha ila yeye alifanikiwa kuokoka katika ajali mbaya ile?"

Inasikitisha sana na inahuzunisha mno watu wamesafiri kutoka mbali na wakati wanapokaribia kituoni na wakiwa na furaha ajali inatokea .Huwa ni vilio vikubwa sana na mara nyiingi watu huweza hata kujiuliuliza kwanini ajali ile inatokea mwisho wa safari na siyo vinginevyo japo ajali haipangwi na haipangiwi.

Maisha yetu ni kama safari ya basi inayotoka sehemu "A" kwenda Sehemu "B".Wakati mtu anataka kufika sehemu B kuna vitu vingi anapitia .Atakutana na vituo ambavyo atasimama kwa muda mfupi na vituo atakavyosimama muda mrefu ili kupata nguvu za kusonga mbele .

Wakati unaendelea na safari ya maisha yako ,kama vile gari linavoweza kupata pancha na mengineyo hata wewe pia katika safari ya maisha yako yapo mengi yanayotokea ambayo yanapaswa kutozuia safari yako .

Jambo moja ambalo linauma ni pale ambapo ulikuwa unataka kufikia ndoto zako ghafla ukaacha ndoto zako kwa sababu yoyote ile.Hii ni hatari sana  inaumiza sana .Ni sawa na mama mjamzito aliyebeba mimba kwa miezi tisa akavumilia lakini akashindwa kuvumilia maumivu ya mwishoni.

Tumekuwa na ndoto nyingi na mambo mengi amabayo tunanafanya /kuanzisha lakini tuavyokaribia kufika mwisho ghafla mambo ya ajabu yanaingilia ili usifike mwisho na mara nyingi mwisho ndo unaangaliwa sana .Jana katiika Moning Rise Up nikwambia kuwa unapaswa kuangalia mwisho kuliko mwanzo .Jitahidi sana kutopotelea mwisho ili ndoto zako ziwe kweli.

Joas(Jyb)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni