"Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni,
umaskini hutokana na matendao ya kila siku ya mwanadamu" (Nelson Mandela,
R.I.P)
"Kila mtu anataka kufanikiwa,
lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye
mafanikio"(Mwl Nyerere, R.I.P).
"Kile unahokifanya muda huu ndicho
kinachoashiria na kutoa picha kamili ya baadae yako"(Mahatma Gandhi,
R.I.P)
"Ukizaliwa maskini sio kosa lako,
ila ukifa maskini hilo ni kosa"(Bill Gate, The richest man in the world).
Mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia
kuwa, "mstari unaomtenganisha maskini na tajiri ni mwembamba sana, kwa
hiyo ni rahisi sana kuwa tajiri pia ni rahisi sana kuwa maskini". Mpaka
leo sijaelewa alimaanisha nini.
Watu wote waliofanikiwa katika nyanja
mbalimbali za maisha, kwenye uongozi, biashara, kilimo, elimu, siasa, michezo,
uandishi, muziki, afya, imani, utangazaji, nk huwa hawana hizi tabia 9 nilizokuandalia
leo, kwa hiyo kama una kiu ya mafanikio kwa hicho unachopambania, achana na
haya mambo 9 yafuatayo;
1.KUTOKUJARIBU. Katika kutafuta
mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita.
"Chagua kufa, au kupambana". "Siogopi kufa, naogopa
kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna alie zaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa.
2.KUTOKUJIFUNZA. Che Guava mpaka
anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, mwenzangu na Mimi sijui
hata kama una Biblia au Quran ghetoni kwako. Nkwameh Nkrumah library yake
ilikuwa na vitabu zaidia ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asbuhi lazima
asome kitu kipya. "JOSEPH=Jifunze, Ona, Soma, Elimika, Pitia,
Hamasika.(Prof Jay)
3.WOGA & WASIWASI. "Tunaweza
tukamsamehe mtoto anayeogopa gizani, lakini sio mtu mzima anaeogopa
mchana"(Plato, R.I.P). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe.
Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho
unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha harali na kia
manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu
ambacho hakijatokea.
4.KUJILINGANISHA. Kuna baadhi ya watu,
huwa wangetamani kuwa kama watu Fulani. Kuwa wewe pia jiamini. Ustamani kuwa
Magufuli, Kassim Majaliwa au Paul Makonda. Kila mtu ni wa pekee na maalumu.
Jikubali kwanza afu wengine ndo watakukubali wewe. Weka nguvu kwenye ubora wako
na sio kwenye madhaifu yako. Ukijilinganisha sana utakosa furaha ya nafsi
maisha yako yote.
5.KUWEKA VINYONGO. "Kuweka chuki na
konyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine".
Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli.
6.UONGO. "Uongo utakupa ushindi wa
siku moja, ukweli utaishi milele"(WEUSI), "Muongo hata akiongoea
ukweli usimuamini"(FID Q). Ukiwa muongo huwezi kufanikiwa hata siku moja.
"Unaweza ukawadanganya watu, lakini huwezi kuwadanganya watu wote, wakati
wote"(Bob Marley). Ukweli kama jua, katika safari ya mafanikio huwezi
kuvificha.
7.UVIVU & UZEMBE. "Nyumba yenye
njaa ukisizi unapata zero"(Fid Q). Mafanikio huja kwa kupenda
unachokifanya. Neno "kazi" katika biblia limeandikwa mara 600.
Dangote analala masaa 3 tu kila siku, Mohammed Dewj anaamka saa 11 asbuhi kila
siku. We kwepa makukumu tu, kesho utakula magodoro. "Uvivu unalipa muda
huu, bidii & juhudi vinalipa baadae".
8.STAREHE & ANASA KUPINDUKIA. Pombe,
sigara, ngono, unga, bange, shisha, cocaine, nk vitu vibaya sana. Ni ngumu sana
kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. "Sisi ni kile tunacho
kula". Mafanikio ya kwanza huanxia kwenye afya yako". Afya ni
utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. "Mavuno ya uzee, ni swaga za
ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana"(Nikki Mbishi,).
9.LAWAMA & UMBEYA. "Watu wenye
uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu
matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu" We upo kwenye
kundi gani? Bora ukawa kundi la kati kuliko hilo la chini kabisa, hilo ni la
"wachawi". Tusilamike, tupambane,lawama hazisaidii chochote.Ukiweka
malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia
ndoto zako
Toa maoni, share pia shauri!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni