Alhamisi, Julai 14, 2016

MAISHA NI MWALIMU


Maisha ni safari ndefu naam katika maisha yapo mengi tunayoona kwa macho yetu na tunayosikia kwa masikio yetu .Yapo mengi ambayo tunakutana nayo katika maisha yetu ya kila siku .Kila jambo katika maisha halipo bure lipo ili tuweze kijifunza kwalo na lijenge maisha yetu na kuyafanya kuwa bora zaidi japo tumekuwa watu wa kupuuza kila aina ya maisha tunayopitia .

Unapoishi na watu katika mazingira fulani wenye hulka,mitazamo na mambo mengine ambavyo viko tofauti na vile ulivyo wewe ni wakati wa kujifunza mengi kutoka kwao na kujua namna ya kuishi nao .Ukiishi na  mwenye hasira ni wakati wa kujifunza mtu mwenye hasira yukoje na kujenga msuli wa kuishi na watu wenye hasira.Ukiishi na watu wapole penda kujifunza kwao na namna ya kuendana nao.

Unapokutana na mtu ambaye humjui mahali popote usimdharau maana humjui .Penda kujifunza kwa kila mtu unayekutana naye utashaangaa unajifunza mengi na pengine akawa chanzo cha maisha yako kubadilika na ukashangaa nini kimetokea .

Wakati tulipokuwa/tunapokuwa shuleni ,vyuoni ,makazini na kwingineko tunakutana na watu wenye malezi tofauti ,mawazo tofauti ,hulka tofauti na tabia tofauti .Katika mazingira kama haya ni fursa nzuri ya kujifunza mambo mengi na kuyachuja ili yakusaidie kuishi na kila mtu hapa duniani .Watu wengi wanashindwa kuishi na watu kwa sababu wanashindwa kujifunza kwa wale wanaokutana nao .

Zipo nyakati ambazo tunapita kwenye shida kubwa na hulka ya binadamu ni kuwa hapendi apitie shida au changamoto.Ushauri wangu ni kuwa unapokuw katika changamoto kubwa na shida kubwa ni wakati wa kujifunza vitu vingi na kujenga msuli wa kuhimili kila gumu unalopitia.Wakati wa magumu ni wakati ambapo akili na uwezo wa kufikiri hukua kwa kiwango kikubwa sana .Ni wakati wa shida ni wakati ambao uwezo wwa kutatua matatizo (problem solving capacity) inakuwa kubwa.

Upo pia wakati unafanikiwa na kuishi maisha ya ndoto yako .Unapofanikiwa ni muda wa kukaa chini na kutafakari na kujifunza sana juu ya maisha na kwanini wewe umefanikiwa na si mwingine .Si wakati wa kuwadharau watu lakini ni wakati wako wa kumfundisha zaidi yule amabaye hajafikia maisha yao .Jua kuwa pamoja na kuwa umefanikiwa kuna mahali ambapo ulipitia na wapo watu waliopo mahali pale ulipopitia na wanahitaji msaada wako wa namna yoyote ili nao watoke mahali walipo .

Joas (Jyb)0753836463/0656110906




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni