UJASIRIAMALI


NAMNA YA KUTUMIA BUTI LA GARI LAKO KIBIASHARA??

Leo nitakuueleza namna ambayo buti La gari lako Unaweza tumia Kama duka na ukawa  unaingiza fedha. Watu wengi wamekuwa wakitumia buti la gari katika Kubeba vitu ambavyo si vya kibiashara.

Lakini Leo Nitakwambia namna ya kutumia buti la gari yako kibiashara.
Unaweza kununua vitenge , Viatu, n. K ukawa unasambaza maofisini na kila unapokutana na marafiki zako.

Kuna wakati unakutana na watu muhimu Ni vizuri ukawa na bidhaa kwenye gari. Beba Juice ya matunda na wauzie wafanyakazi. Beba viungo, bidhaaa za makampuni yanayofanya kazi kwa mtandao Kama Umejiunga  n. K.

Mara nyingi tumekutana na watu wengi katika matukio mengi na tumekosa fursa kwa uzembe wetu.

Leo Fikiria namna ya kufanya buti lako liwe kiuzalishaji zaidi.

KWA MAWAZO YA KIBIASHARA NITAFUTE WATSAP 0753836463



*********************************************************************************


"MAMA HUYU HUPATA MILIONI MOJA NA NUSU KWA MWEZI AKIUZA CHAPATI MIA KILA SIKU"

Akili yako ndo utajiri wako au umaskini wako !

Mama mmoja ambaye hakutaka jina lifahamike aliamua kuanza kutengeneza chapati na kuziuza eneo la Posta (watu husema mjini).

Mama huyu hutengeneza wastani wa chapati mia moja kila siku na kuzisambaza maofisini ambapo kila chapati huuzwa sh 500 /=.kwa hiyo akiuza chapati zake zote 100 hupata sh elfu hamsini kwa siku na kwa mwezi hupata milioni moja na nusu .

Mama anasema "Natembelea ofisi kwa ofisi na kama ofisi nizotembelea zina watu 5 wenye uwezo wa kuchukua chapati mbili maana yake nitapita kwenye ofisi kumi tu na chapati zangu zinakuwa zimeisha  na kujipatia elfu hamsini".
Huamka asubuhi na mapema kuwahi watu wanaotafuta vitafunwa maofisini ,kama unavojua Watnzania ni wavivu wanapenda vya kuletewa .Sasa uvivu wako ni fursa kwa mwingine .
Mama humaliza kuuza chapati majira ya sa nne asubuhi na hurudi nyumbani kwake kuendeleza genge .Mbali na chapati huuza pia mihogo,sambusa n,k maofisini na zingine huacha kwake .Mama huyu hutengeneza kipato kikubwa sana kwa siku na kwa mwezi hukusanya zaidi ya milioni mbili.

Endelea kuamini unachokiamini huku ukiendelea kuwa maskini jeuri .Chapati ni zaidi ya mishahara yako ya miezi mitatu.Kwanini usiuze chapati ??????????

Usikose makala za fursa na ujasiriamali kila alhamis

Kamata fursa .
Joas(Jyb)  Watsap 0753836463


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni