STORI

SIMULIZI YA NICK VIJICIC MLEMAVU ASIYE NA MIGUU WALA MIKONO ANAYEFANYA MAMBO MAKUBWA 

Nick Vujicic ni Muastralia aliyezaliwa bila miguu wala mikono lakini kuzaliwa kwake hivo hakujazuia kuishi kusudi lake.Kwa sasa ana miaka 32 na ni mwanzilishi wa Taasisi ya maisha bila miguu na ni muhamasishaji ,huwapa matumaini wale wenye ulemavu ,ameoa na mtoto mmoja.

Nick anasema "Naamini kuna sababu ya kwanini kitu kinatokea .Fanya kila unaloweza bila kukata tamaa huku ukimwamini Mungu .Nilizaaliwa na mtazamo huu namshukuru Mungu kwa kila nilichonacho .Wazazi wangu hawakunilea tu katika Uzuri lakini pia walikuwa jasiri kupata watoto wengine "

Anaendelea kusema "Mama yangu alikuwa Mkunga na hivyo alifijua fika kuhusu maswali ya uzazi .Alijua fika kuwa mimba yake ilikuwa na shida wakati niko tumboni.Alipiga utrasound zote .Nilivozaliwa watu wengi walistuka kuona sina Miguu wala mikono"

"Asubuhi siku ya kuzaliwa kwangu .Baba alikuwa amekaa pembeni ya mama na aliona kuwa mabega yangu hayakuwa na mikono .Alitaka kuzimia na kutapika ilibidi Muuguzi ampeleke nje .Ukweli ni kwamba sikuwa na mikono wala miguu na madaktari walishindwa kueleza chochote kuhusu tatizo hilo" .Alisema Nick

Nilikuwa mlemavu wa kwanza kupelekwa kwenye mfumo wa shule wa Australia .Nilinyanyaswa na kutengwa sana shuleni kwa hali niliyokuwa nayo .Wazazi wangu waliniambia kuwapuuza  watu walionibeza .

Kila mtu anatafuta kitu cha kumfanya afurahie maisha .Nilitaka kujua kama mimi si wa kufa tu .Kila mara mtoto akinicheka au kunitenga hofu ilinijaa na nilikimbia kwenda nyumbani .

Nilipokuwa na miaka 10 nilitaka kujiua .Nilihisi sina thamani na nilifikiri nitaendelea kuwa mzigo kwa wazazi wangu na kamwe nikadhani sitakuja kuoa .Hii iliendelea mpaka pale nilipoona mvulana ambaye naye alikuwa hana mikono wala miguu kama mimi .Nikajua kumbe siko peke yangu .

" Ninaogolea ,kuvua samaki na kufanya mambo mengi kama kuperuzi kwenye mtandao na mengineyo  " alisema Nick .Kama Kijana nataka kuwa huru kadri iwezekanavyo.Wazazi wangu waliniambia "hujui unaloweza kufanya mpaka pale utakapojaribu ".Naweza kupiga mswaki na kuosha nywele zangu .Katika mazingira yoyote nafanya kadri ya uwezo wangu .Maisha siyo kile ulichonacho lakini ni vile unaweza kukitumia kile ulichoncho .Siogopi kujaribu na kushindwa.

Nimetembelea nchi 58 na maili milioni 3 (hii siyo kudanganya).Ninamshukuru Mungu nimekuwa nikiongea na viongozi wa Dunia akini pia yatia na wale wote waliosaulika na kuonekana hawana faida kwa jamii.

 .Nilianza kuhamasisha wengine Australia nikiwa na miaka 19 na kisha nikitambea duniani ndani ya miaka mitano.Nina ndugu Califonia na wamekuwa wakinitia moyo nisonge mbele ."Nick ,unaweza kufanya ndoto zako ziwe za kweli na kuufikia ulimwengu mzima ".Nilianza maisha bila miguu wala mikono


Nick anajifunza kucheza mchezo wa Gofu . Anasema " siogopi kujaribu na kushindwa ",hii ndo staili ya maisha yake .Akiongea na vijana huwa anafurahisha sana .Anatengeneza mwelekeo na maisha yenye thamani na kusui kwa vijana .Anasema kuishi kwenye familia maskini ni mbaya sana kuliko kutokuwa na miguu.

Nick anasema nataka watu wasiogope .Siyo vile ulivyo kwa nje lakini vile ulivyoumbwa kuwa ndo kitu cha msingi kwenye maisha ."Umetunikiwa ,una kipaji na mambo mengi amayo yako ndani yako"

Nilioa .Mke wangu Kanae ni ni chotara (mjapani-mmarekani ) na nilikutana nae kwenye Tax .Ilikuwa ni mara ya kwanza napenda.Tulimshukuru Mungu kwa kukutana .tulienda taratibu bila yeye kuacha masomo aliyokuwa akisoma .

Miezi mitatu baadae mwaka 2011 tukiwa katika mahusiano nilipata shida binafsi .Nilienda kuazisha biashara na biashara hiyo haikuweza kusonga mbele .Niliibiwa pia fedha niliyokuwa nayo .Niliwaomba wazazi wangu fedha kwa kuwa niikuwa nimeibiwa na sikuamini kuwa katika umri wa miaka 28 ningekuwa mzigo tena kwa wazazi wangu .Nililia sana .

Sikuamini kuwa Kanae Angeendelea Kunipenda na kubaki nami .Alisema " ni sawa tu mume wangu ,siwezi kwenda kokote .nitatafuta kazi ya uuguzi (nursing) .Hapa ndipo nilipoamini kuwa kweli Kanae alikuwa mke wangu.

Miezi tisa baadae nimvisha pete ya uchumba .Na baada ya mwaka mmoja tulioana na Kiyoshi mtoto wetu akazaliwa .Yeye ananifika kwenye mabega na huwa tunakumbatiana na kubusiana kila siku.

Nawaambia watu wasikata tamaa.huwa tunasubiri miujiza kutokea katika maisha yetu lakini muujiza hauji kamwe.Natamani vitu vingi vingebadilika katika maisha yangu .Nikijua kuwa mimi naweza kuwa chanzo cha muujiza kwa mwingine naishi maisha yenye tija na yenye kusudi.

Nick anamaliza kwa kusema "Wote tuna hofu .Mimi siyo zaidi .Lakini jikubali na fuata kile kilicho cha muhimu na maana katika maisha yako."

FUATILIA MFULULIZO ZA SIMULIZI ZA WATU WANAOFANYA MAMBO MAKUBWA
HAPA HAPA  



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni