Ni ukweli
usiopingika kuwa huwezi kumzuia kuku jike kutaga mpaka hapo utakapo
mchinja.Lakini akiwa bado yuko hai hakuna namna utaweza kumzuia kuku huyu kutaga.
Wengi
yawezekana hawaamini hili kwa kwa kuwa hawajawahi kufuga kuku lakini kwa wale
waliobahatika kufuga kuku hilo jambo wanaliewa.
Nilpokuwa
mtoto nilikuwa mtundu na mdadisi japo si sana.Niliwahi kufanya majaribio kadhaa
kumzuia kuku asitage nikaambulia ola maana kuku huwezi mzuia kutaga kivyovyote.Mama
yangu alikuwa mjasiriamali wa kijijini kwa wakati huo kupitia ufugaji wa kuku.
Wakati kuku
akiwa anataka kutaga huwa anahangaika ,anazunguka zunguka kupata mazingira
mazuri ya kutagia na mara nyingi hupendelea kutagia bandani.Sasa fanya kama
unafunga banda kwa kufuri ili asitage ,kuku huyu utakuta katagia kwenye nyumba
ya kulala watu .
Kuku huyu huyu
anapoona nyumba na mazingira ya karibu siyo wezeshi kwa yeye kutaga ,hukimbilia
nyumba ya jirani na utasikia majirani wazuri wanakwambia "Aise fulani kuku
wenu huwa anatagia kwetu na tayari ameshataga mayai kadhaa".
Kuku huyu huyu
anapoona mazingira ya jirani yamemgomea yeye kutaga yai lake zuri linalomsumbua
,huenda kichakani na kutaga huko bila kujali chochote kama vile mayai yake
kuliwa na wanyama na hata yeye mwenyewe kuliwa(ana roho ngumu).Huchukua maamuzi
ya kijasiri kupata yai lake moja tu .
Kuku huyu
nataka nimfananishe na binadamu ambaye ameona fursa ,ana ujuzi na mambo
kedekede lakini utamsikia akisema mazingira haya siwezi kufanya chochote huku
akitoa sababu za kushindwa kutekeleza jambo hilo(iga kuku mtetea).
Watu wamekuwa
wanataja sababu kedekede ya kwanini wamedhindwa kufanikisha jambo fulani lakini
ukweli ni kwamba hujafikiri kwa kina namna ya kulifanikisha(rejea kwa kuku
mtetea).
Fursa uiyonayo
sasa itazaa makubwa(mayai) na sasa kama utashindwa kutekeleza na kuingia moja
kwa moja kwenye utendaji maisha yako yataendelea kuwa yale yale na utakuwa
wimbo wako wa kila siku.
Umekuwa mtu wa
tahadhari nyingi katika kujaribu kila mzaingira na kuku amekushinda akili maana
kuku huenda mpaka vichakani anapoona mazingira ya nyumbani yameshindikani na
kule kichakani hafikirii kingine lakini hufiikiria yai lake .
Naomba mayai
yetu(fursa) tusizipoteze ati kwa sababu ya mazingira
(watu,vikwazo,mitaji n.k).
Narudia kusema
Huwezi kumzuia kuku kutaga labda umchinje .
Joas(Jyb)
Ni hazuiliki kuku hazuiliki
JibuFutaakuna mtu anahe weza kuzuulia kuku kutaga kamwe au hivi una weza kuuzuwia mbuzi kuzaha au nipeni jibu kwa sasa please
JibuFuta