Huwa nashangaa
jinsi ambavyo mara zote mti ukikatwa huwa unachipuka tena .Hata hivyo napata
jibu kuwa mti siyo matawi lakini ni mbegu iliyopandwa chini na ikatengeneza
mizizi ambapo mizizi hiyo isipong'olewa mti lazima utaota tena hata kama
ukikatwa.
Naamini hata
wewe uliwahi kukata mti na ukadhani kuwa hautaweza kumea tena na ukashangaa
kuona kuwa mti umechipua tena kwa uzuri na kwa kustawi kabisa pengine kuzidi
hapo awali .
Kuna wakati
pengine watu walitaka /wanataka kukatisha ndoto zako na maono yako ili usifikie
mahali Mungu amekutakia kufika ,watu hawawezi kukatisha ndoto zako maana Mungu
alishawekwa mizizi ya kufanikiwa kwako na hakuna namna utakavoshindwa kuchipuka
tena na kufikia hatma ya maisha yako .
Kuna watu
wanaotamani upitie kwenye changamoto kubwa na uannguke vibaya ili wakucheke
lakini ninachoamini n kuwa haijalishi utaanguka mara ngapi lazima usimame tena
maana unao uwezo na nguvu za kuinuka na Kusonga Mbele .
Nguvu yako
haiko kwenye vitu vinavyoonekana na unavyomiliki (matawi) ,nguvu yako na uwezo
wako viko ndani yako na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuviondoa mpaka hapo
utakapoamua mwenyewe na huo ndo utakuwa mwisho wa ndoto zako .
Ukweli ni huu
kwamba watu wengi wanatamani usifanikiwe na kusonga mbele na wamejiandaa na
mapanga yao ili ukkatwe.Mapanga yao ni maneno ya kukatisha tamaa,vikwazo n,k .Hata hivyo hawataweza kama unajua uwezo
ulio nao ambao ndio unakupa uwezo wa kusonga mbele na kuendelea kufanya.
0753836463/0656110906
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni