Jumatatu, Juni 06, 2016

HAPO ULIPO HUJAFIKA



Ndugu yangu,Ipo kawaida ya mtu kurizika na mahali alipo au mafanikio aliyonayo hata kama ni madogo.


Mimi nasema kama unamiliki genge unapaswa kutoka kwenye biashara ya genge .kama unamiliki duka unapaswa kuwa na supermarkert kubwa .Vile vile kama una kampuni moja unapaswa kuwaza kumiliki makampuni na viwanda .

Ukweli ni kwamba binadamu ana tabia ya kujisahau na kuamini kuwa hapo alipo ndo mwisho wake.Umesababisha ubongo kulala na kutowaza mbali zaidi na matokeo yake maisha yamekuwa hayabadiliki .Maisha ya miaka 5 iliyopita mwaka juzi ndo ya mwaka huu .

Maisha ni hatua  kama binadamu alivo na hatua za ukuaji .Mtoto anayatambaa ,wazazi hufurahi anapoanza kutembea.Ndugu maisha sasa yamekuwa yenye ushindani mkubwa na wale wenye nguvu(financial stability) ndio wanaoinyanyasa dunia .Ekolojia inasema kuwa maisha yanafuata kanuni ya "survive for the fittest " kwamba wale wenye nguvu ndio wanaoishi.


‪Joas‬(Jyb)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni