Mpendwa
Naamini umzima !
Waswahili
husema "samaki mkunje angali mbichi" na "udongo uwahi ungali
maji.Mimi nataka nifaninanishe samaki na udongo kama wazo zuri la kibiashara
ulililonalo wewe.
Mara
nyingi Mungu amekuwa akawapa mawazo mazuri watu lakini huwa si
watekelezaji(doers) wa mawazo haya kwa wakati na huwa huchukua Muda kutekeleza
mawazo mazuri na pengine huwa mawazo yanakufa kabisa au mtu anatoweka (kufa)
bila kuweka wazo lake kwenye utendaji .
Myles
Mnuroe aliyekuwa mshauri wa kufikia mafanikio makubwa na Mhubiri wa Injili
Wengi tutakuwa tunamfahamu (Nasikitika hatunaye sasa) alisema "When God
see the Graves ,he wipes" akimanisha kuwa Mungu akiyatazama makaburi
anasikitika kwa watu wamekufa na utajiri mkubwa vichwani mwao.
Ndugu
yangu hakuna Muda mzuri kama sasa,waswahili husema “liwezekanalo leo,lisingoje
kesho”.Msemo huu unamanisha kuwa kama una nguvu ya kufanya jambo leo lifanye tu
kwa uwaredi maana kesho yako hauijui.Unaweza kusema nitafanya kesho ,kesho afya
yako isiwe vizuri kulifanya.
Lameck
Amos Hulilo Mkurugenzi wa Mpango Mkakati Technologies alitambua sili hii ya
nguvu ya sasa/leo.Lameck kila alipopata wazo ,mara moja aliliweka katika
utendaji.Kumbuka wazo la kwanza la Lameck ilikuwa kutengeneza Bussiness card
akiwa chuo na aliliweka kwenye utendaji na akafanikiwa bila kusubiri eti
mazingira yamsaidie.
Huna
sababu ya kutoweka wazo lako kwenye uhalisia .Anneth Isaya Gerena ambaye
tuliweza pata simulizi yake Kijana Jithamini watsap group alilitambua hili japo ni Kiziwi .Anneth
anasema "Mwaka 2010 January niliendelea kutafuta kazi bila mafanikio
nilituma karibu application Mia lakini wapi.... February 2010 nikakaa chini na
kutafakari, nikajisemea nguvu ninazo, elimu ninayo, maarifa ninayo, ujuzi ninao
sasa kwa nini nihangaike kiasi hiki kutafuta kazi???? Nitatafuta mpaka lini? Nitawategemea wazazi na ndugu hadi lini??????.Nikamuomba sana Mungu anipe
ujasiri wa kufanya kitu katika maisha yangu kiwe suluhisho LA kuhangaika huko
na kule kusaka kazi bila mafanikio..... Basi nikajikaza sikuwa na hata senti
moja tuseme niite mtaji.Nikaamua kuwakusanya wanawake viziwi wenzangu ambao
hawakuwa na elimu wala ajira kabisa mwenye Elimu nikiwa mimi pekee yangu...
NikawAmbia mimi mwenzenu nimemaliza chuo lakini sijabahatika kupata kazi Lakini
nina kitu nataka kuwafanyia ili kuwakomboa pamoja na kujikomboa mwenyewe....
Huo ndo ukawa mwanzo wa asasi ya furaha ya wanawake wajasirialiamali kwa viziwi
Tanzania, FUWAVITA I am the founder and director of that NGO “
Wakati
unasema huna mtaji Lameck Amos ambaye ni Mkurugenzi wa Mpango Mkakati
Technologies hakuwa na Mtaji kama wewe leo anamiliki Kampuni yake , Francis
Lutufyo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Digital gates naye alianza hivo lakini
pia Dada Anneth Isaya Gerana hakuwa na mtaji lakini yeye pia alikuwa mlemavu
lakini alifanya kitu.Wewe uko fit asilimia 100% ,una mazingira mazuri,
unasubiri nini???.
Nimalize
kwa kusema ipo nguvu katika maamuzi magumu yako unayofanya sasa.AMUA KUFANYA
KITU LEO:
- Amua kuuza genge
- Amua kuanzisha kampuni
- Amua kuanzisha duka
- Amua kufanya mradi wowote
- Amua kutembeza nguo
- Amua kupiga picha na kuziuza
AKUTAKIAYE KUFANIKIWA KATIKA MAISHA YAKO
Joas(Jyb)
0656110906
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni