Jumamosi, Juni 04, 2016

Wewe ndiwe mwenye Kuwajibika na Maisha yako




"Yohana 5:7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ."

Kuna wakati mwingine tunapitia mateso na shida na tunakuwa tunadhani kuwa ndugu  zetu  na marafiki zetu wanaweza kutusaidia na tunapokosa msaada huwa huwa tunaingiwa roho za chuki na vinyongo maana wao walikuwa watu wa kututoa mahali tulipo  bila kujua kuwa maisha yetu ni yetu binafsi .

Yawezekana unapitia kwenye shida na taabu mbalimbali na huna mtu wa kukutoa.Ni kweli inauma unapoona wanaokuzunguka hawakusaidii wakati huo wao wakiwa na uwezo wa kukusaidia .Hupaswi kukuta tamaa ,songa Mbele kazana huku ukiwa unamuomba Mungu akutoe mahali ulipo .

Dunia ya leo imegeuka na inahitaji jitihada binafsi kutoka mahali ulipo na kiukweli  .Watu wapo wachache watakaokusaidia katika wakati ukiwa katika changamoto.

Mfumo wa kuzaliwa peke yako ni kwamba utawajibika mwenyewe katika kuishi kwako na hata mapacha huwa wanatofautiana muda wa kuzaliwa ,hii ni kwasababu kila mtu ataishi maisha yake .Kama ukipata Neema ya mtu kukutoa mahali ulipo shukuru Mungu lakini ukweli sisi ndio madereva wa maisha yetu

Joas  (Jyb)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni