Alhamisi, Julai 14, 2016

KWANINI UJUTE ??

Waswahili husema majuto ni mjukuu wakimanisha kuwa mtu hujuta baada ya kupata hasara .Watu wengi sasa wameishi maisha ya kujuta na hawana tumaini la maisha yao .

  • watu wanajuta kusoma chuo fulani
  • watu wanajuta kusomea masomo fulani
  • watu wanajuta kuolewa au kuoa mtu fulani
  • watu wanajuta kwa maamuzi ambayo waliwahi kufanya. n.k
Kujuta ni matokeo ya maamuzi ambayo tulidhani ni sahihi hapo awali lakini baadae tukagundua kuwa maamuzi yale yalikuwa si sahihi na sasa hakuna namna tena ya kufanya .Kama hii ndo sababu ipo haja sasa ya kuwa na umakini wa kila tunaloifanya katika maisha yetu na maamuzi ya kila siku ambayo tunafanya .

Nakutana na watu ambao wanajuta ati kwanini hawajaenda shule wakati huo wao ndo walikuwa sababu ya kutokwenda shule kwa makusudi na sasa wanajuta Wamesahau kuwa maisha ya binadamu hayajirudii na daima tupatapo nafasi ya kufanya jambo tunapaswa kulifanya tukijua kuwa nafasi hii haitajirudia tena (life is irrevisible)

Kujuta ni matokeo ya maamuzi ambayo tulidhani ni sahihi hapo awali lakini baadae tukagundua kuwa maamuzi yale yalikuwa si sahihi na sasa hakuna namna tena ya kufanya .Kama hii ndo sababu ipo haja sasa ya kuwa na umakini wa kila tunaloifanya katika maisha yetu na maamuzi ya kila siku ambayo tunafanya .

Kuna watu hujuta baada ya kustaafu kazi na kuona kuwa na kujikuta kuwa hajafanya  chochote juu ya hatma ya familia yake ilihali alikuwa na nafasi kubwa ya kufanya vitu vikubwa wakati bado hajasataafu .Huu ni Ugonjwa ambao umewaathiri watu wengi  sana  na unapaswa kuwa makini sana wewe unayesoma makala hii.

Kuna watu wamezungukwa na fursa nyingi na wanashindwa kuzitumia huku wakidahani kuwa kila siku fursa zitakuwepo na wamesahau msemo ule unaosema kuwa opportunity never come twice (nafasii haiji mara mbili).Siku wakistuka na kutaka kufanya mambo wanakuta fursa ile haipo tena na wananza kujuta .
Ushauri wangu ni kuwa ni vizuri kutumia kila fursa unayokutana nayo maana wewe usipoitumia fursa yupo mtu atakayeitumia na utajuta kwanini hukuitumia fursa ile kwa wakati ule .

Kuna watu wana nafasi ya kufanya vitu vikubwa na mawazo makubwa lakini kwa makusudi hawafanyi chochote na kuweka mawazo yao kwenye utendaji na utawasikia wakisema  watafanya kesho,keshokutwa ,mwakani utafikiri yaliyoko mbele wanayajua .Ndugu amka nafasi ni hii usije ukajuta.Nani kakwambia kesho utakuwa na nguvu kama ulizo nazo leo????

Ukweli ni kwamba sisi ndio wasababishaji wa majuto katika maisha yetu .Tumekuwa watu wakupuuzia vitu vidogo na kufanya maamuzi yasiyo sahihi tusijue kuwa yana madhara makubwa .Kuna umuhimu sasa wa kuanya mambo kwa uangalifu mkubwa kuepuka majuto.

Jyb(0753836463/0656110906)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni