Moja ya tofauti kubwa kati ya watu
Maskini na matajiri ni juu ya matumizi ya
muda .Maskini hana nidhamu katika matumizi ya muda na hivyo hudhani kuwa muda
alionao utaendelea kuwepo na hivyo huutumia
vibaya wakati huo tajiri hutumia vizuri kila sekunde anayoipata .
Ukiwauliza watu waliofeli kwenye
mitihani ya kidato cha sita yaliyotangazwa jana kujua kipi kimepelekea wao kufeli ,wengi
watakueleza kuwa Muda wa kidato cha tano na cha sita ni mdogo sana na mambo ni
mengi .Hii ndiyo tabia ya mtu anayeshindwa na maskini ambaye kila siku huleta
visingizio .
Kwa upande Mwingine ukiwauliza watu
ambao wamefaulu sana katika matokeo atakwambia kuwa moja
kati ya vitu ambavyo vimepelekea wao kufaulu vizuri ni kuwa walitumia muda vizuri
baada ya kuona kuwa vitu ni vingi na na hivyo kutumia muda mwingi katika
kujisomea .
Ukichunguza na kupata ukweli kwanini
watu wengi ni maskini ,utangundua kuwa maskini
hutumia muda mwingi sana kwenye starehe ,mapumziko hata kama hajafanya
kazi, kupiga stori na kuwaongelea watu wengine(umbea) .Maskini hutumia muda
mwingi kulaumu wengine huku wasijue kuwa wanapoteza muda.Kumbuka hao unawaoongelea wanafanya yao ya kujenga maisha yao
Matajiri huwa ni watu ambao hutumia muda
katika mambo yenye tija .Huwekeza sana muda wao kupata maarifa (kusoma vitabu
,kuangalia video zenye kuwaendeleza n.k).Matajiri hufuata ratiba zao
walizojiwekea na siyo bendera kufuata upepo .
Mungu alitoa masaa 24 kwa kila mtu
,shida inakuja kwetu kwa namna tunavyotumia muda .Muda huwa siku zote unatosha
isipokuwa wengi tunakosa uelekeo na kufanya yale ambayo hatukupanga kufanya
.Tumekuwa watu wa kuyumbishwa na ratiba zetu wenyewe na tumekuwa bendera fuata
upepo .
Utawezaje kutumia muda wako vizuri??
1.Andika vitu utakavyofanya kesho kabla
hujaenda kulala
Kutojua kesho utafanya nini ni hatari
sana na ndio sababu kubwa inayopelekea unapoteza muda mwingi kwa kufanya mambo
yasiyo na tija .Ni muhimu sana kama unataka kufanikiwa uwe na tabia ya kuandika
yale yote ambayo utafanya vinginevyo utafanya lolote na kukuta kuwa siku
imeisha bila kufanya mambo ya msingi .
2.Weka vipaumbele
Ni muhimu baada ya kuandika utafanya nini kujua
vipaumbele vyako ni vipi kwa siku hiyo.Mambo yote uliyoyaandika yanaweza yakawa
siyo yote ya msingi .Unashauriwa kuanza kufanya yale ambayo ni ya muhimu sana
.Hii inakusaidia kumaliza mambo yote ya muhimu kwa siku hiyo .
3.Weka Nidhamu kwa uliyoyapanga
Kuandika utakachokifanya inaweza kuwa
rahisi sana lakini shida kubwa iko kwenye kufuata kile ulichokiandika.Hakikisha unajenga nidhamu kubwa juu ya mambo ulijiwekea mwenyewe .Acha kabisa kufuata
ratiba za watu wengine .Fuata mambo yako.
Ndugu huwezi jua thamani ya kitu mpaka
pale utakapokipoteza na kutoweza kukipata tena .Muda huwa hauwezi kujirudia
(Time is non renewable resource).Watu wamejikuta wakijuta kuwa kama wangelijua
wangelitumia muda vizuri .Siamini kama hawa wanaojuta hawakujua kuwa muda ni
Mali .Amka sasa jiwekee utaratibu mzuri wa kutumia muda(time management).
Jyb (0753836463/0656110906)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni