Tunaishi katika dunia ambayo fikra hasi
zimetawala .Watu wamekuwa karibu sana na fikra zao hasi kuliko uhalisia wa
jambo.Fikra hasi umekuwa ugonjwa wa kuambukiza na sasa umeathiri sehemu kubwa
ya maisha ya watu wengi sana duniani hasa vijana na hivyo kupelekea
ndoto zao kuyeyuka na sasa hawana tumaini la maisha yao ya kesho.
Watu wamekuwa wakiamini kila kinachoingia
masikioni mwao bila hata kufanya mchujo wa nini kinafaa na kipi hakifai kwa
mstakabali wa hatma ya maisha yao.

Vijana wamejiingiza katika madawa ya
kulevya kujiuza wenyewe kwa sababu ya fikra zao hasi na kukataa tamaa ya
kuishi .Hofu ya wasichokijua
imekuwa kikwazo kikubwa na imepelekea vijana wengi kutodhubutu mambo mbalimbali
ya kuleta maendeleo badala yake wamebaki wakilaumu ndugu zao na hata serikali
kwamba haijawasaidia .
Fikra hasi zimewafanya vijana wengi kukaa
bila kazi wakati wana uwezo na vipaji mbalimbali .Wamekuwa wakibagua kazi na
kuchagua kazi zenye mishahara mikubwa na sasa umasikini na maisha magumu ndo
wimbo wa kila siku kwao.
Dunia sasa imekuwa na vijana lukuki ambao
hawana kitu cha kufanya lakini wakiwa na nguvu kubwa na uwezo mkubwa wa
uzalishaji .Hali hii imekuwa mbaya zaidi katika nchi zilizopo chini
ya jangwa la sahara na tatizo linaendelea kukua kwa kasi kila iitwapo
leo.
Fikra hasi zimepofusha watu wengi na sasa
wameshindwa kuona fursa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua kutoka katika lindi la
umaskini.
Vijana wengi wasomi wanatoka vyuoni na
fikra hasi za kuajiriwa tena kwa mishahara mikubwa na badala yake wanakaa muda
mrefu wakitafuta hizo kazi za mishahara mikubwa na hawazioni na mwisho wanabaki
kulalamika bila kutafuta majibu na sasa elimu yao imekuwa
Elimu makaratasi na wengi wao sasa wameanza kuitwa wasomi hewa .
Familia zetu zimekuwa zikijenga watoto
katika mitazamo hasi bila kumfanya mtoto kuwa mbunifu na pengine kulea kipaji
cha mtoto ambacho anaweza kukionesha wakati wa ukuaji .
Wazazi pia wamekuwa wakiwachagulia watoto
masomo ya kusoma badala ya kuwaacha watoto kufuata ndoto zao .

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wakati akiwa
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni aliwahi kusema yafuatayo akiwa katika uzinduzi
wa maonyesho ya tano ya Tanzania Homes Expo yaliyoandaliwa na Kampuni za EAG
Group jijini Dar es Salaam. “Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo kama vijana wangezitumia zingeweza kuwapatia
ajira na kuondokana kukimbilia nchi jirani kujihusisha
na uuzaji wa dawa za kulevya na kuishia kutofikia malengo yao. Fursa hizo
zimekuwa zikichangamkiwa na wageni ambao wanatengeneza malighafi kwa kutumia
rasilimali za hapa nchini.
Vijana
wengi wanakimbilia nje ya nchi wanaziacha fursa na kushindwa kukuza uchumi wa
nchi.
Kwanini
vijana wengi wana mitazamo hasi??
- Marafiki wabaya walio nao : vijana wameshindwa kujua kuwa maisha haya yanatokana na watu waliokuzunguka .Na kama unazungukwa na watu wenye mtazamo hasi basi hata wewe utakuwa hivo hivo .Vijana wengi sasa wameshindwa kuwa na jicho la tatu ya kujua nani na kwanini anapaswa kuwa rafiki yangu.
- Vitabu wanavyosoma: Kimuuingiacho mtu ndicho kimtokacho .Ni dhahiri kuwa vitu tunavosoma kwenye vitabu vina athari kubwa kwenye maisha yetu .Vijana wengi wamekuwa wasomaji wa vitu ambavyo haviwajengi .Vijana wengi hupenda vitabu vya mahusiano kuliko vitabu vya kuwaletea maendeleo yao na vinavyojenga maadili.
- Vitu anavyosikiliza: Runinga zetu na radio zetu zina athari kubwa kwenye maisha yetu ya kila siku .Vijana wamekuwa wakisikiliza sana nyimbo za kuamsha mapenzi kwa muda mwingi badala ya kusikiliza vitu vya msingi vya kujenga maisha yao.
- Mfumo wa Elimu yetu:Mfumo wa elimu pia umesababisha kuwajenga watu kuwa na mitazamo hasi ya kuamini kuajiriwa kuliko kutumia uwezo ulioko ndani ya mtu katika kuzalisha na kutengeneza ajira kwa wengine.
- Mapokeo: Vijana wengi huamini katika kile walichokikuta katika familia zao ,nchi yao n.k. Huamini kuwa maisha ni bahati na nyote jambo ambalo si sahihi .
KWA USHAURI NA MAWAZO NITAFUTE KWA NAMBA HIZI
![]() |
0753836463 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni