Jumamosi, Julai 16, 2016

KANUNI NNE (4) ZA KUFIKIA MAFANIKIO YAKO


Mafanikio siyo ajali na siyo nyota bali ni mchakato wenye utaratibu.Huwezi kulala leo maskini ukaamka kesho tajiri ikitokea hivo huo ndo utakuwa mwisho wa dunia .Mafanikio ni matokeo ya uwekezaji wa muda na mambo yanayofanana na hayo .

 Leo nakuletea hatua nne ambazo kama ukizifuata na kuzitilia manani zitakufikisha kwenye mafanikio unayoyatamani .Hatua hizi ni za kidunia na zimetumiwa na watu wengi ambao walishafanikiwa .

1.KANUNI YA KUSABABISHA NA KUATHIRI(LAW OF CAUSE & EFFECT)

Wale ambao wamekuwa wakifuatilia makala zangu niliwahi kusema kuwa ili uweze kufanikiwa lazima uwe ni mtu unaweza kufanya vitu vitokee na kuathiri mazingira .Unapokuwa ukifurahia umeme ujue unafurahia mawazo na matokeo ya Thomas Edison aliyeumiza kichwa na kushindwa mara nyingi lakini sasa tunafurahia umeme .Kuna watu wanadhani umeme ni wa Tanesco kumbe ni wa mtu mmoja aliyewekeza muda wake na kusababisha matokeo.

Acha kabisa kusherekea matokeo ya wengine huku ukiwa na nafasi ya kufanya mambo makubwa .Kwanini hujiamini?? kwanini huoni uwezo ulionao???.Mafanikio yako kwenye uwezo wako wa kufanya vitu vitokee.Azimia leo kuwa mtu wa kufanya vitu vitokee na si kushangilia watu wengine .

2.KANUNI YA KUAMINI (LAW OF BELIEF)

Jana nilikuwa naongea kwa simu na rafiki yangu Yakobo Mumbe Kijana mdogo ambaye sasa ni mmiliki wa huduma ya Gospel Campaign For The whole World ambaye mara nyingi huwa yuko South Africa kihuduma akawa anieleza jinsi anavyooamini huduma yake kufika mbali sana na kufika au kuzidi viwango vya akina Pator Joel Osteen, Pastor David Oyedepo,Pator Chris na wengineo .Hii ni Imani kubwa na uamini mkubwa wa ndoto yake .

Ili ufanikiwa lazima uwe ni mtu wa kuamini ndoto yako .Wewe ni ndiwe pekee unayeweza kufanya ndoto yako iwe kweli au kiukwamisha .Kwanini unashindwa kuamini mawazo yako mwenyewe na kuamini mawazo ya wengine?? , kwanini unashiindwa kuamini uwezo wako na unataka kuamini mawazo ya wengine .Hey ! Amka wewe usinziaye utaachwa .

3.KANUNI YA MATARAJIO (LAW OF EXPECTATION )

Brian Teracy katika kitabu chake cha 100 laws of business success anasema "You are always acting as a fortune teller in your own life by the way you think and talk about how the situations  are going to turn out"  akimanisha kuwa wewe ni kama mbashiri unayeweza kujibashiria namna ambavyo mambo yako yatakuwa badae hata kama hujui .Ukitaka kufanikiwa lazima utarajie matokeo makubwa ya kile unachokiamini .Unapotarajia kushindwa lazima utashindwa tu na kama unatarajia kushinda utashinda.

Siri ni hii unapotarajia kushinda unazalisha nguvu ya ziada ndani yako(Enthusiasm ) ndani yako na hakuna litakalo kuzuia kufanya lile unalofikiria kulifanya .


4.KANUNI YA SUMAKU  (LAW OF MAGNET)

Kile ulicho nacho na vile ulivyo ni matokeo ya vitu ulivyovivuta kuja kwako , vile unavyowaza na watu wanaokuzunguka .Chochote unachotaka unauwezo wa kukivuta kije kwako maana wewe ni kama sumaku .Brian Teracy anasema "Whatever you want ,wants you " kwamba kila unachokitaka kinakutaka .

JYB(0753836463/0656110906)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni