
Leo nakuletea hatua nne ambazo kama
ukizifuata na kuzitilia manani zitakufikisha kwenye mafanikio unayoyatamani
.Hatua hizi ni za kidunia na zimetumiwa na watu wengi ambao walishafanikiwa .
1.KANUNI YA KUSABABISHA NA KUATHIRI(LAW
OF CAUSE & EFFECT)
Wale ambao wamekuwa wakifuatilia makala
zangu niliwahi kusema kuwa ili uweze kufanikiwa lazima uwe ni mtu unaweza kufanya
vitu vitokee na kuathiri mazingira .Unapokuwa ukifurahia umeme ujue unafurahia mawazo na matokeo ya
Thomas Edison aliyeumiza kichwa na kushindwa mara nyingi lakini sasa
tunafurahia umeme .Kuna watu wanadhani umeme ni wa Tanesco kumbe ni wa mtu
mmoja aliyewekeza muda wake na kusababisha matokeo.
Acha kabisa kusherekea matokeo ya
wengine huku ukiwa na nafasi ya kufanya mambo makubwa .Kwanini hujiamini??
kwanini huoni uwezo ulionao???.Mafanikio yao yako kwenye uwezo wako wa kufanya
vitu vitokee.Azimia leo kuwa mtu wa kufanya vitu vitokee na si kushangilia watu
wengine .
2.KANUNI YA KUAMINI (LAW OF BELIEF)
Jana nilikuwa naongea kwa simu na rafiki
yangu Yakobo Mumbe Kijana mdogo ambaye sasa ni mmiliki wa huduma ya Gospel Campaign For The whole World ambaye mara nyingi huwa yuko South Africa kihuduma
akawa anieleza jinsi anavyooamini huduma yake kufika mbali sana na kufika au
kuzidi viwango vya akina Pator Joel Osteen, Pastor David Oyedepo,Pator Chris na wengineo .Hii ni Imani kubwa na uamini mkubwa wa
ndoto yake .
Ili ufanikiwa lazima uwe ni mtu wa
kuamini ndoto yako .Wewe ndiwe pekee unayeweza kufanya ndoto yako iwe kweli
au kiukwamisha .Kwanini unashindwa kuamini mawazo yako mwenyewe na kuamini
mawazo ya wengine?? , kwanini unashiindwa kuamini uwezo wako na unataka kuamini
mawazo ya wengine .Hey ! Amka wewe usinziaye utaachwa .
3.KANUNI YA MATARAJIO (LAW OF EXPECTATION )
3.KANUNI YA MATARAJIO (LAW OF EXPECTATION )
Brian Teracy katika kitabu chake cha 100
laws of business success anasema "You are always acting as a fortune
teller in your own life by the way you think and talk about how the
situations are going to turn out" akimanisha kuwa wewe ni kama mbashiri
unayeweza kujibashiria namna ambavyo mambo yako yatakuwa badae hata kama hujui
.Ukitaka kufanikiwa lazima utarajie
matokeo makubwa ya kile unachokiamini .Unapotarajia kushindwa lazima utashindwa
tu na kama unatarajia kushinda utashinda.
Siri
ni hii unapotarajia kushinda unazalisha nguvu ya ziada ndani yako(Enthusiasm )
ndani yako na hakuna litakalo kuzuia kufanya lile unalofikiria kulifanya .
4.KANUNI
YA SUMAKU (LAW OF MAGNET)
Kile
ulicho nacho na vile ulivyo ni matokeo ya vitu ulivyovivuta kuja kwako , vile
unavyowaza na watu wanaokuzunguka .Chochote unachotaka unauwezo wa kukivuta
kije kwako maana wewe ni kama sumaku .Brian Teracy anasema "Whatever you
want ,wants you " kwamba kila unachokitaka kinakutaka .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni