Asubuhi hii nikiwa kwenye gari , nikiwa
natafakari Juma lilinavyoanza ghafla nikaanza kuwaza maajabu haya ya dunia .Ndiyo
kwangu mimi ni maajabu japo wewe unaweza kuona kawaida .
Starter ambayo wenzangu na mimi wanasema
“stata” ni kitu cha ajabu sana .Kwa wasiofahamu starter huwa kwenye magari
,pikipiki ,tubelights n.k. starter ndo husaidia uanzaji wa gari na vifaa
vinavofanana na hivyo.Usione magari makubwa na mazuri yanapita barabarani bila
starter hayawezi kwenda kuwaka na kwenda kokote .
Nilipokuwa nasoma masomo yangu ya Olevel
,madarasani tulikuwa tunatumia tubelights .Wakati wa maandalizi (Prepo) wale
wanafunzi wasiotaka kujisomea na wavivu walikuwa wanapenda kuchomoa starter
kwenye tubelights hizo na wakishachomoa tubelights zilikuwa zinashindwa kuwaka.Wanafunzi
hawa wazembe wa kujisomea Walijua fika bila starter wale ambao walikuwa
wanasoma kama wametumwa na vijiji vyao wasingeweza kujisomea .
Anyway nisiongelee sana stori lakini
point yangu hapa ni kwamba maisha yako yako kwenye kuanza .Unahitaji sana
starter yako mwenyewe(self-starter) ili ufike unapotaka kwenda .Ukiona mtu
hafanyi kile alichopanga kufanya ujue huyo starter yake imechomolewa .
Siri ya watu waliofanikiwa walikuwa na
uwezo wa kuanza vitu maana walikuwa wana starter zao wenyewe na walipogundua
kuna watu wanataka kuficha starter zao walikuwa makini sana na leo wamefika
mbali .
Jana Rafiki yangu Lameck Amos Hulilo
muhitimu wa masomo ya uhandisi wa chuo kikuu cha Dar es salaam katika masomo ya
uhandisi wa tarakirishi (computer) mwaka 2014 ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni
ya Mpango Mkakati Technologies iliyoko eneo la Ubungo Dar es salaam alitueleza
kwenye kundi la Kijana Jithamini kuwa pamoja na kwamba sasa anamiliki Kampuni
yake binafsi lakini ameanza huduma ya kutoa chakula ambayo yeye ameiita kwa jina la EAT &
SAVE (Kula na uokoe pesa).Lameck ni mtu mwenye nguvu kubwa ya kufanya maamuzi
yake mwenyewe katika kuanza jambo (self-starter) .Big up kwake .
Mpendwa bila kuwa na nguvu ya kuanza
jambo hutafanya lolote katika na maisha yako na utakufa ukiwa umewaachia mzigo
wanaobaki kwa mipango yako mingi iliyoandikwa kwenye makaratasi .Nani kakwambia
ili uanze unahitaji kuwa na milioni moja??? Nani kakwambia ili uanze unahitaji
kuwa mtu maarufu ??? .Hee hujui Huyu Lameck alianza kutengeneza Business card
za watu??? .Come on unajua hapo ulipoajiriwa huyo mkurugenzi alianza na mtaji
kiasi gani??? .Shida siyo mtaji shida ni kukosa starter yako mwenyewe .
Jyb (0753836463/0656110906)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni