Jumatatu, Julai 18, 2016

HAYA NDIYO MALENGO YA MWENDOKASI


Baada ya Ujio wa magari yaendayo kasi maarufu kama Magari ya mwendokasi hapa jijini Dar es salaam, neno mwendokasi limekuwa ndiyo habari ya mjini kwa muda sasa.Utasikia watu wanasema ana kiatu cha mwendokasi , ana urefu wa mwendokasi kila kitu sasa kimekuwa cha mwendokasi .

 Upo umuhimu wa kuwa na malengo ya mwendokasi katika maisha yetu ya kila siku.Malengo ya mwendokasi ndiyo malengo tunapaswa kwenda nayo katika karne hii ya 21 yenye mabadiliko makubwa na changamoto nyingi.

Kwanini Malengo ya Mwendokasi??

Ukiwa na Malengo ya mwendokasi lazima ndoto yako itimie maana hakuna atakayeweza kuzuia.Hutarusu watu wakupunguzia mwendo.

 (You will be unstoppable).

  • Ukiwa na Malengo ya mwendokasi yatakulazimisha kuamka usiku na kuanza kuyatekeleza hata kama usingizi ni mtamu kiasi gani (you will be with passion
  • Ukiwa na malengo ya mwendokasi hutaacha kutafuta maarifa  kila siku na kwa gharama yoyote kama yaliyopo hapa ou will seek knowledge)
  • Ukiwa na malengo ya Mwendokasi utatumia muda kwa makini sana .(you will spend your time wisely )
  • Ukiwa na malengo ya mwendokasi yatakufanya uwe unjifanyia tathimini mwenyewe kila baada ya muda.(being able to do self evaluation) 
Ili Malengo yako yawe ya mwedokasi lazima yafuate sifa hizi ambazo si ngeni kwako :


  • Malengo lazima yawe mahususi(specific) : Ni muhimu sana kujua nini hasa unataka katika maisha yako .Huwezi kufanya kila kitu lazima kuna mambo machache unaweza kufanya kwa uzuli hayo ndiyo uyaandike .
  • Malengo lazima yapimike(measurable): Ni muhimu kuweka malengo yaliyo ndani ya uwezo wako baada ya kutathimini uwezo binafsi wa kufanya mambo .Jipime kishe ujiwekee malengo yako.
  • Malengo lazimaa yawe yakufikika(Attainable): Ni vizuri kuweka malengo ambayo utaweza kuyafikia na uweke mikakati ya kuhakikisha unayafikia .Ni kosa kubwa kuweka malengo ambayo unajua hutaweza kuyafika 
  • Malengo lazima yawe halisia (Realistic) :Ni muhimu sana malengo yako yakawa yenye kubeba uhalisia wa jambo unalotaka kulifanya .
  • Malengo lazima yawe na Ukomo(Time bound):Kila jambo lina mwisho wake.Hakikisha malengo yako unayawekea muda .Bila kuwa na ukomo wa muda hutafanya chochote na malengo yako yataishia kwenye makaratasi au njiani.

0753836463






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni