Jumatatu, Julai 25, 2016

JIFUNZE KWA MTEGAJI Na; Joas Yunus




"Mtegaji huwa si lazima anase siku hiyo hiyo aliyoweka mtego."

Hapana shaka kuwa  unamfahamu mtegaji  ni nani na wengi wetu twaweza kuwa tuliwahi kumtega hata panya nyumbani kwetu.

Malengo ya wategaji huwa yanatofautiani kulingana na matakwa ya mtegaji.Wengine hutega panya kwa sababu panya wanamharibia mazao.Wengine hutega kwa ajili ya kupata kitoweo(Nyama)

Hata hivyo ili Mtego uweze kunasa hutegemea mambo yafuatayo kama yamezingatiwa na mtegaji; 

  1. Eneo alilotega: Siyo kila eneo linafaa kwa utegaji hivyo mtegaji huangalia mahali pazuri ambapo ni rahisi kunasa .
  2.  Namna alivyotega: Utaalamu katika utegaji nao huwa ni jambo la kuzigatia maana ukikosea huweza kunasa.:
  3.     Kivutio alichoweka kwenye mtego wako:iIli unasa lazima uweke kitu ambacho humvutia yule ambaye umelenga kumnasa
Mtegaji hutembelea mara kwa mara mtego wake kuona  kama umenasa .Na kama haujanasa huwa anabadilisha eneo,kubadilisha mfumo wa utegaji ama kuongeza vivutio kwenye mtego ili anase.

Mtegaji hana kawaida ya kuacha kutega tena au kung'oa mitego yake ati kwa sababu wiki imeisha bila kunasa lakini hukaa na kufikiri ni  jinsi gani atanasa.

Watu wengi  tumekuwa tukijaribu kufanya mambo mbalimbali ili tuweze kufanikiwa .Tumekuwa tukianzisha vitu na mara tunavooona hatupati kile tulichodhani kama tungepata tunaachana na kitu hicho .Hii ni tabia ya watu wengi wa chini ambao mara zote wao hukata tamaa mapema mara wanapokutana na Changamoto.

Wakati mwingine umeanzisha duka lako na hujapata wateja siku tatu unawaza kuachana na Biashara badala ya kuwaza kubadili mfumo wako wa biashara na namna ya kuwafanya wateja wavutike na Biashara yako .Wakati mwingine umedhani kama biashara yako imelogwa kumbe mchawi wa biashara yako ni wewe mwenyewe .

Kuanzisha kitu tu haitoshi lakini inahitaji mambo mengi sana .Biashara nyingine haiendi labda kwa sababu ya eneo ulipo ,utoaji mbaya wa huduma (Huduma kwa wateja) ,kukosa nidhamu ya biashara n.k

Haupaswi kungo'a mitego au kuacha kabisa kutega .Angalia ulichokosea katika utegaji .Kama hutanasa leo Jua utanasa kesho kama unafuata kanuni za utegaji .


Joas 0753836463

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni