Jumanne, Julai 26, 2016

Rubani hupotezwa au kusaidiwa na waongozaji wa ndege



Ndugu msomaji wa makala hii!
Leo nataka kugusia jinsi rubani wa ndege anavyopotezwa na waongozaji wa ndege (Air Traffic Controllers) .

Waongozaji wa ndege ni wataalamu wa mambo ya anga na hukaa kwenye chumba maalumu wakiwasiliana na Rubani juu ya usalama wa Anga na hali ya hewa ya anga ili kumsaidia Rubani kuweza kuifikisha ndege salama.

Ni wazi kuwa kama Muongoza ndege hatawasiliana vizuri na Rubani na kumpa taarifa sahihi za anga ,kuna uwezekano ndege ikapata shida njiani.Hivyo umakini wa muongoza ndege na mawasiliano mazuri na Rubani huifikisha ndege salama .

Ndugu ,unaweza kuona sasa jinsi ambavyo Muongoza ndege ana mchango mkubwa katika kuhakikisha ndege inafika salama au isifike salama.

Ajali nyingi ulizowahi kusikia ni makosa ya mawasiliano na taarifa za anga ambazo si sahihi kutoka kwa waongoza ndege.

Unapaswa kujua kuwa kwenye maisha yetu ya kila siku kuwa  wewe ndo rubani wa ndege yako inayokupeleka kwenye uwanja wa mafanikio na wapo wanaoogoza ndege yako au wanataka kuongoza ndege yako ya Mafanikio unapaswa kuwa nao makini maana wanaweza sababisha kufika au kutokufika.

Watu wenye kiu ya kutaka wewe ufanikiwe,wanaokuonesha mbinu za kufanikiwa , wanaokushauri n,k hawa ni waongozaji wazuri na watakufikisha mahali unapokwenda japo changamoto njiani utazipitia.

Wapo wale waongozaji wengine ambao ni waongozaji wabaya ambao hawataki wewe ufanikiwe na mara nyingi ni watu wa kukukatisha tamaa na kukuvunja moyo hawa una kila sababu za kutowasikiliza maana ndege yako ya mafanikio haitafika.

Leo una maamuzi ya kuchagua nani anapaswa kuwa Muongozaji wa ndege yako ya mafanikio ambaye atahakikisha ndege yako kufika  inakokwenda kinyume na hapo utaishia njiani .

Joas(Jyb)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni