Kuna wakati fulani kwenye kundi la
kijana Jithamini watsap (Waweza kujiunga kwa kutuma namba yako hapa 0753836463) niliwahi uliza swali hili "Mkulima A alipanda mbegu
katika shamba B lakini mara kadhaa mkulima huyu alikuwa
havuni kwa miaka mingi sasa .Nini unaweza mshauri ?"
Watu kadhaa waliweza kuchangia nini
zinaweza kuwa sababu za kukokosa mavuno na haya yalikuwa baadhi ya majibu :
Christina moja ya manachama wa kijana
jithamini anasema "nitamshauri asikate tamaa ajaribu tena coz mjasiriamali
ni risk taker kwa habari ya kilimo inawezekana alifuata hatua zote na eneo lina
tutuba ya kutosha ila mvua ikanyesha zaidi
kama mwaka huu au ikawa pungufu "
Mabula Jilala mwamdishi na mmiliki wa
Morning Tanzania blog anasema"kama mvua zilinyesha kuna mambo kadhaa
huenda yalisababisha :
1. Mvua ilizidi sana ikayaharibu
2.Udongo haukuwa na rutuba au ulikuwa haufai
kwa mbegu hizo
3.Hakutumia wadudu waharibuo mazao ya
mahindi "
Abdulnuru mwanachama wa kijana jithamini
anasema"awe anafanya reseach kabla hajaanza kulima coz sio mazao yote
yanakubali kila mazao "
Majibu yote yalikuwa mazuri na yanaweza
kuwa sababu ya mkulima kushindwa kuvuna (kupata mazao).Mfano huu una maana
kubwa katika maisha .
Mkulima hapa anafananishwa na mwajiri na
mbegu ni mwajiriwa na shamba linafanishwa na kampuni/taasisi ambayo mwajiriwa
huyu kaajiriwa.Ukweli ni kwamba unapoajiriwa kwenye kampuni au taasisi yoyote
umepandwa na sasa kama wewe umepandwa kampuni tunategemea tuone mavuno(maisha
yabadilike).
Kuna mtu anakaa miaka 10 hadi 15 kwenye
kampuni maisha hayabadilii(hakuna mavuno) hii inamanisha umepandwa katika
shamba ambalo silo .Hata kama unapata mshahara maisha hayabadiliki,akili
imedumaa na mawazo yamekwazuliwa,huna amani wala furaha .Tatizo hapo ni kuwa
umekosea shamba na unapaswa kutafuta shamba mbadala ili uvune . shamba lako
mbadala labda ni Kipaji kinachoweza kuutajirisha au hata viinginevyo .Wakati
mwingine mbegu zinakuwa nzuri lakini shamba likikosewa hakuna kitakachovunwa .
Ushauri wangu ni kuwa ni muhimu sana
kufanya tathimini ya nini kimeongezeka maishani mwako wakati ukifanya kazi
katika kampuni A au taasisi.Maisha ni mafupi sana yatupasa tuanze kuona mavuno yenye tija.
Joas(Jyb)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni