Jumamosi, Julai 30, 2016

"BILA VYETI UTAISHI"?

Moja ya sababu zinazofanya kuwepo kwa kundi kubwa la watu ambao hawana ajira ni imani zilizojengekeka juu ya elimu za darasani ambazo hulenga kutoa vyeti badala ya kumtengeneza mwanafunzi kupambana na mazingira.Uliwahi kujiuliza kama tungekuwa tunasoma bila vyeti ungeishije?

Ukweli ni kwamba wakati nasoma sikuwa naamini kuwa mtu mwenye shahada ya pili (Master degree ) anaweza kosa kazi.Lakini ukweli ni kwamba kuna watu wengi wenye shahada ya pili na hawana kazi.(Shida ni nini?)

Shida ni kwamba vyeti  tunavyopata vinatufanya tutengeneze matabaka na kuwa na makundi kadha wa kadha japo hatuna uwezo sawa na vyeti tulivyonavyo .Nakumbuka wakati nasoma shahada ya Kwanza chuo kikuu cha Dar es salaam sehemu ya mlimani kulikuwa na matabaka ya kozi tunazosoma .

Wakati huo Mtu anayesoma uhandisi alijiona bora kuliko mtu anayesoma kozi yoyote ile lakini ukweli ni kwamba huyu mtu wa uhandisi akiingia mtaani  anaanza kuhangaika kutafuta kazi  maana elimu aliyonayo ni  nadharia na hawezi kuonesha ubunifu wa kihandisi.

Ni elimu za vyeti zimetufanya tuchague kazi za kufanya hata kama mtu  hana kazi yoyote kwa muda huo .Nani aliyekwambia mtu mwenye shahada hawezi uza chips? .Elimu zetu zitusaidie kufanya vitu wanavyofanya watu wengine lakini  kwa ubora zaidi .

Ushauri wangu ni kuwa pamoja na kwamba tunaenda shule ni vizuri tukayatafuta maarifa .Maarifa ndo yanayotufanya tuishi hata kama mazingira hayawezi kupokea vyeti tulivyonavyo.wewe ni shahidi kuna walimu wamemaliza toka mwezi wa saba mwaka jana na mpaka sasa hawajaajiriwa.Ukifanya utafiti wa kujua nani anajihusisha na chochote kabla hajapata hiyo ajira ni wachache sana .Wengi wanalaumu tu kuwa serikali imechelewesha ajira badala ya kutumia eimu aliyopata .

Elimu bila Maarifa haitakusaidia :
  1. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.(BIBLE)
  2. Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.(BIBLE)
  3. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uweo(BIBLE)
  4. Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji ya maarifa .(BIBLE)

  Joas 0753836463





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni