Alhamisi, Agosti 11, 2016

MAMBO YA KUFANYA UNAVOHISI KUKATA TAMAA





Moja ya sababu kubwa inayofanya mtu asifanikiwe ni kukata tamaa .Mara nyingi mtu anapotafuta kitu bila mafanikio kwa muda mrefu hukata tamaa ya kuendelea kutafuta kitu hicho na hatimaye kushindwa kukipata kitu hicho.

Watu wengi huwa wanapenda kufikia mafanikio makubwa lakini ni wachache wanaofanikiwa .Wengi huishia njiani kwa sababu ya kukata tamaa.Miongoni mwa vitu vinavyosababisha tukate tamaa ya kupata kile tunachokitaka ni :
   1.Mitazamo yetu
   2.Mazingira(watu wanaotuzunguka n.k)

Mambo haya yatakusaidia pale ambapo utahisi kukata tamaa :

1.*Angalia mwisho wako* : Ukihisi kama unakata tamaa ni muhimu kuangalia ni kitu gani utapata kama hutakata tamaa na kama utashinda changamoto unazopitia .Angalia ni faida kubwa kiasi gani utapata kama hutakata tamaa .Ni kama mama mjamzito anavyosubiri kuzaliwa kwa mtoto na hivyo changamoto za kulea mimba huwa hazimsumbui.Kama ukiendelea kuangalia mahali ulipo leo badala ya kuona utapokuwa miaka mitatu au mitano ijayo lazima utakata tamaa.

2.*Epuka vipunguza mwendo:*  Achana na marafiki wenye mtazamo hasi na wasiotaka wewe kupiga hatua .Watu hawa ni vipunguza mwendo ambao kila siku watakuwa wakikueleza sababu ambazo zitakufanya usifanikiwe katika maisha yako hata kama wewe unaona unaenda kufanikiwa .Vipunguza mwendo siyo watu wa mbali anaweza kuwa ndugu yako au rafiki yako wa karibu .

3.*Jisemee moyoni kuwa "Hii ni kwa leo tu "*. Brian Tracy aliwahi kusema kuwa kama unapitia changamoto kubwa kwa siku ya leo unapaswa kujisemea maneno haya " this is just for today " .Changamoto unazopitia leo kesho zinaweza kutokuwepo na ikawa ndo siku ya kufanikiwa kwako .Amini kuwa kesho lazima litachomoza tena .

4.*Jua kuwa hauko peke yako* : Maisha tunayopitia kuna watu tayari walishayapitia na hivyo unapaswa kujua wewe siyo peke yako .Jifunze kwa waliofanikiwa na utajua kuwa changamoto unazopitia kuna watu walipitia zaidi ya hizo unazopitia

5.*Jua kuwa Hofu Inadanganya* : Unapaswa kujua kuwa hofu ni adui mkubwa wa mafanikio .Hupaswi kuogopa kushindwa ,Amini una uwezo mkubwa ndani yako na hakuna chochote kinachoweza kukuzuia maana wewe huzuiliki .

6.*Tafuta Mshauri wako* : Ni vema ukawa na mtu wako wa karibu na siyo lazima awe ndugu yako ambaye unaweza kumwambia changamoto unazopitia .Ni muhimu mtu huyo akawa mtu mwenye mtazamo chanya na ambaye amepita ulikopita 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni