Somo: Unadhani unachelewa au umechelewa?
Mwl. Kelvin Kitaso, 0713804078
Watu wengi
hushindwa kufurahia kwa kutokana na hali ya kudhania kuwa wanachelewa. Wengine
wamekuwa na papara katika maisha na kufanya vitu visivyoeleweka kwa kudhania
kuwa wanachelewa au wamechelewa. Uvumilivu ni kitu cha msingi sana na
kitakusaidia kutokuwa na papara. Wengi wakiona marafiki zao wanamiliki magari
wanajidhania wamechelewa na hulazimika hata kukopa mikopo ili tu na wao wanunue
magari.
Nani kakuambia
umechelewa, nan i kigezo gani kinakuonyesha unachelewa? Achana na hali hiyo na
uanze kufanya mambo kwa utulivu na utaratibu.
Mambo Yanayoweza Kumkumba Mtu Anapojidhania Kuwa Amechelewa au
Anachelewa.
· Kufanya mambo kwa kukurupuka.
·
Kuishi kwa msongo wa mawazo,
akili inakuwa haina utulivu.
·
Kusababisha gharama zisizo za
msingi kwa sababu tu ya kukurupuka na kufanya vitu kwa pressure.
·
Kuanza kufanya mambo na kuishia
katikati na kughairi tena kufanya.
·
Kukosa msimamo, na maamuzi
mengi hufanya kulingana na upepo wa wakati huo unavyoenda.
·
Kuvutwa na upepo wa kila jipya
linaloingia. Hapa ndipo unakuta mtu kila kikundi kikianzishwa yeye humkosi,
kila biashara ikiingia utamkuta anajaribu, biashara za mitandao zimekuwa nyingi
ila kila zikiingia yeye anajiunga kwa sababu anadhani amechelewa sasa
anajitahidi kuwahi.
Wengine
wanatafuta kazi sana na wanafika mahali wanaombwa rushwa ya fedha au ya ngono
na hujikuta wanatoa kirahisi kwa kuwa wanadhani wamechelewa. Kumbe ungejizuia
kutotoa rushwa kazi yako ingekuja tu kwa wakati wako, kujidhania kwako kuwa
unachelewa ndiko kuna sababisha unapita njia ya mkato.
Wengi
wanapita katika njia zisizo sahihi kwa kudhania kuwa wakipita katika njia
zilizo halali wanachelewa, ila njia zisizo halali hazina Baraka. Ukweli ni
kwamba bora ukawie kufika ila ufike salama kuliko kuwahi kufika ila si salama
(yaani umefika tayari umetengeneza kovu). Njia za mkato kweli zinakufikisha
kule unapotaka kufika ila si salama. Usijidhania kuwa umechelewa au unachelewa,
wewe vumilia tu kupitia katika njia iliyo salama.
Nini ni alama
ya kuchelewa kwako? Unaposema kuwa umechelewa kuoa au kuolewa nini ni alama
inayoonyesha kuwa umechelewa au unawahi? Au unaposema umechelewa kupata kazi
nini ni alama ya kuchelewa kwako ambayo ukiiangalia utasema ndiyo kiashiria cha
kuchelewa kwako. Watu wengi katika maswali ya hapo juu utasikia wakijibu kuwa
yaani marafiki zangu wote wameoa au wameshaolewa, au marafiki zangu niliosoma
nao wote wameshapata kazi. Kipimo chako kikiwa ni wanadamu utaishi kwa kuteseka
sana katika maisha haya. Kipimo chako mfanye kuwa ni Mungu. Maana ratiba za
Mungu si sawa na wanadamu. Wanadamu wanaweza kusema kuwa ukiwa na miaka 23
unatakiwa uwe umeolewa na sasa una miaka 27 bado hujaolewa unajihisi kukata
tamaa na kushuka kwa kuwa unadhani ulipaswa kuolewa ukiwa na miaka 23, hiyo ni
kanuni za wanadamu tu ambao wao ufikiria hivyo ila inawezekana wewe umepangiwa
kuolewa ukiwa na miaka 32. Kwa wanadamu umechelewa sana, ila katika ratiba za
Mungu huo ndio wakati mwafaka.
Mungu
hatakutendea jambo kwa kuwa kawaida za wanadamu zinasema hivyo, Mungu
atakutendea kwa sababu wakati wake wa kukutendea umefika, na ndio maana kwa
Mungu mwanamke wa miaka 90 anapata mimba, ila kwa sisi wanadamu mwanamke wa
miaka 50 hawezi kupata mimba. Hii tafsiri yake ni kuwa muda wa Mungu si muda wa
mwanadamu.
Unadhani Sara
na Ibrahimu walichelewa kupata mtoto? Watu wengi huwa wanadhani kuwa Sara na
Ibrahim walichelewa kupata mtoto kwa kuwa alipatikana wakiwa wazee sana. Ukweli
ni kuwa kwa Mungu, Sara na Ibrahim hawakuwahi wala kuchelewa kupata mtoto ila
walipata ndani ya wakati sahihi. Yaani wanadamu walikuwa wakiwashangaa ila ule
ni wakati wa Mungu kwao. Hata wewe haujachelewa, wanadamu ndio wanakuaminisha
uone kuwa umechelewa. Mungu ni Mungu wa majira na wakati.
Wanadamu sisi
tunaamini kuwa mtu akimaliza tu chuo ndio wakati sahihi kwa Yeye kupata ajira,
na mtu akikaa miaka 2 na kuendelea bila kazi tunasema kuwa amechelewa kupata
kazi, na hata yeye huamini kuwa amechelewa na anachelewa kufanya maendeleo
haswa anapowaona wenzie wakifanikiwa. Jambo la msingi kufahamu tena ni kuwa
bado hujachelewa, Mungu anaratiba anayoijua juu yako.
Ukisoma katika
kitabu cha Yeremia 29:11, Mungu anasema najua mawazo ninayowawazia, ni mema na
wala si mabaya. Mara zote Mungu anayo mawazo yaliyomema, anayo ratiba iliyo
njema maishani mwako na kwamwe hautachelewa.
“Kwa
kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” Mhubiri
3:1
Katika biblia
kuna habari za mwana mpotevu aliyemuomba baba yake ampe sehemu ya mali zake
akafurahi nchi ya mbali, na aling’ang’aniza kupewa japo haukuwa wakati wake ila
alikuwa na papara za kupata kwa wakati ule, alipopewa alienda kuzitumia vibaya
na kufuja na mwisho wa siku alirudi akilia akiwa amechoka na hana hata kimoja
katika vile alivyoondoka navyo kwa baba yake.
Usiwe na
papara, fanya kwa sehemu yako kwa juhudi zote na umuachie Mungu akamilishe
makusudi anayoyataka. Usimtangulie Mungu, mwache akutangulie.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni