SOMO:
MALEZI YA MTOTO (SEHEMU YA KWANZA)
NA:
MWALIMU KELVIN KITASO ..... 0713804078
Suala la malezi ya
mtoto katika wakati huu limekuwa ni suala lenye changamoto kubwa sana kutokana
na maendeleo ya sayansi na teknolojia na pia mwingiliano wa watu wa jamii
mbalimbali kutoka katika mataifa mbalimbali ya pande zote za dunia
(utandawazi). Na mtazamo huo wa malezi umekuwa na muingiliano mkubwa sana na
maandiko Matakatifu katika makuzi ya mtoto kwa kupanga yale yaliyonenwa katika
maandiko, hii ni mbinu ya shetani kutaka kuchafua kizazi ili kiwe nje ya kusudi
la Mungu katika kumlea mtoto. Shetani hujitahidi sana kutumia watu wakubwa
katika dunia hii kuleta mawazo yanayopingana na Biblia akijua kwa kufanya hivyo
ataweza kujipatia wafuasi wengi kwa kufanikiwa kukiharibu kizazi.
“Mlee
mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”. Mithali
22:6. Maandiko Matakatifu yanasisitiza juu ya kumlea mtoto katika njia impasayo
kwa kuwa hataiacha hata atakapofikia uzee wake, na pia ukimlea mtoto katika
njia isiyompasayo hatoiacha pia hata atakapokuwa katika uzee wake.
Kumlea mtoto ni suala ambalo Mungu
ameweka kwa mzazi na hakuishia tu kuliweka mbele ya mzazi bali alitoa namna
gani mtoto huyo anapaswa kulelewa. Dr. Mayles Munroe anasema, “marejeo mengi uweka wazi kuwa watoto hujifunza kila kitu
wanachotaka kufunzwa katika miaka saba (7) na kushuka chini. Baada ya miaka
saba (7) hujifunza yale tu wanayotaka kujifunza; kwa maana nyingine, kama
haujamfundisha mtoto katika njia impasayo katika miaka saba (7) ya kwanza na
kama haujamuambukiza tabia yako, mwenendo wako na mambo yako katika wakati huo
ni vigumu sana hata neema ya Kristo isaidie baada ya miaka hiyo. Lakini kama
umefanikiwa kumuonyesha njia impasayo katika umri huo wa miaka 7, hakika
wataweza kuifuata njia hiyo katika siku zote za maisha yake. Wanaweza kujaribu
tabia nyingine kama wanavyofanya watu wengine lakini mwisho wake watakumbuka
yale mafundisho waliyowahi kuyapata na kurudi tena.”
Ukweli ni kwamba
mtoto katika umri wa miaka 12 na kuendelea si rahisi sana kuiga kila kitu
kutoka kwa wazazi na mara nyingi upenda kujaribu kufanya yale ambayo wanaona
wengine wanafanya na hata yale wakatwazayo kwa kuambiwa kuwa ni mabaya, wao
upenda kuyajaribu ili wajihakikishie wao wenyewe kuwa yana ubaya au hayana.
Katika umri wa miaka hii na kuendelea mtoto uenenda kutokana na vile
alivyokuzwa akiwa chini ya umri huo na yale mafundisho aliyoyapata umsaidia
kwenda vizuri. Ndio tafsiri ya msemo usemao ‘mtoto umleavyo ndivyo akuavyo’.
Wazazi wengi wapo
katika majuto makubwa ya tabia za watoto wao, ila ukiangalia chimbuko ni msingi
waliowawekea wao wenyewe toka wakiwa wadogo. Msingi ulio imara ujengwa katika
neno la Mungu. Mzazi ni lazima awe na juhudi kubwa ya kumlisha mtoto wake neno
la Mungu tangu akiwa mdogo, angali katika tumbo la mama yake kwa kumtamkia
maneno ya Mungu na yaliyo ya ushindi, neno li hai na tena lina nguvu kubwa,
halipingwi na mipaka ya mfuko wa mama alipo mtoto katika tumbo, lenyewe upenya
na kwenda kuumba yale maneno yaliyotamkwa kwa imani. Azaliwapo na aendeleapo
kukua hakikisha unafanya juhudi kubwa ya kumlisha neno la Mungu likae kwa wingi
ndani yake, naye ajue kulisema na kulishika kwa uzuri kwa kuwa hataliacha hata
atakapokuwa mzee na ni lazima lizae matunda mema kwake ambayo utayafurahia.
Msidanganyike
wazazi, ni neno la Mungu tu, ndilo uweza mfanya mwanao awe salama na kuokoka na
dunia hii iliyojaa na uovu wa kila namna. Dunia ipo kwenye hali mbaya sana na
inawimbi baya sana liwezalo kumpoteza mtoto wako hata kama amezaliwa katika
familia ya ukristo wa viwango vikubwa sana; ukiwekeza kumfundisha neno ni
lazima awe mtu wa tofauti sana na utamfurhia kwa mwenendo mwema wa kufurahisha.
“Moyoni mwangu
nimeliweka neno lako nisije, nikakutenda dhambi,” Daudi anazungumza ni kwa nini
ushindwa kumtenda Mungu dhambi, ni kwa sababu ya lile neno ambalo lipo ndani
yake umkumbusha mara zote nini yaliyo mapenzi ya Mungu kwake. Neno likikaa kwa
watoto ndani yao vyema hawatamtenda Mungu dhambi na pia litawasaidia kuwa na
nidhamu bora katika jamii.
Ibilisi amekuwa na
udanganyifu mkubwa sana hata ndani ya watumishi wa Mungu kwa kutia ushawishi
kuwa mtoto uwa haokoki ila wanaookoka ni wazazi tu na mtoto anaokoka akisha
kuwa mtu mzima, huu ni udanganyifu mkubwa uliofungwa ndani ya walio wengi sana
kwa kuwa maandiko uonyesha habari za Timotheo alianza kumcha Mungu tangu akiwa
mtoto mdogo, Daud, Yusufu, Isaka, Yeremia, Samweli na Yesu walianza kumcha na
kumtumikia Mungu tangu wangali wadogo kwa kuwa neno la Mungu liliwafikia tangu
walipokuwa wadogo. Udanganyifu huu unasababisha watu wajitie moyo kuwa wakikuwa
na kujitambua na wao wataookoka, si kweli kwa kuwa wanahitaji neno mapema kabla
mambo hayajaanza kuharibika.
Waswahili wanasema “samaki mkunje angali mbichi.,” kwa
kumaanisha kuwa hata mtoto uweza rekebishwa na kutengenezwa tabia akiwa katika
umri mdogo bado kwa kuwa hakishakuwa mkubwa ni vigumu sana kumrekebisha mtoto
kama huyo. Mtoto ni kama samaki mbichi makuzi na maisha yake ya baadae utegemea
ni kwa namna gani unamfanya kabla hajakua/kauka.
Watoto hawawezi
kujikuza wao wenyewe na ndiyo maana wazazi na walezi wapo ili kuwakuza. Kwa
mtoto kuwa vizuri katika maeneo yote ya maisha ni matokeo ya mafunzo anayopata
kutoka kwa wazazi na walezi. Zipo shule na taasisi mbali mbali zenye kuwafunza
watoto na nyingine uwasajiri toka wakiwa wadogo sana na kuanza kuwalea, ila
mlezi mkuu na mwenye dhamana kuu ya kulea ni wazazi wa mtoto, na ni vigumu
kuona mtoto yupo kama utakavyo wewe kama ukumlea wewe.
Mtoto yeyote yule
akuzwaye katika makuzi mazuri, ukua kwa kumpendeza Mungu na wanadamu na uwa
furaha pia kwa wazazi wamkuzao mtoto huyo, kwa maana mtoto mpumbavu ni mzigo
kwa mamaye ila mwana mwenye hekima ni utukufu kwa wazazi wake.
Dunia inalia na
haina majibu juu ya kumlea mtoto katika njia impasayo na wasomi na watafiti
wengi wamefanya utafiti na kugundua kuwa makelele, fimbo ya adhabu na ukali
mwingi kwa mtoto si njia njema ya kumkuza mtoto, wakati ulimwengu unayo maswali
mengi yupo Mungu ambaye kwake hakuna lisilowezekana na kwake malezi bora
inawezekana lakini pia vitu hivyo havitoshi hususani fimbo ya adhabu pasipo
kujumuishwa na neno la Mungu ambalo ni sababu kubwa ya mabadiliko kwa mtoto.
Ni ukweli kabisa
kuwa wapo wazazi wengi sana ambao wametumia muda wao mwingi kupiga makelele kwa
watoto wao kuhusu tabia mbaya na wengine wamekuwa wakali sana na uogopwa kila
wakati wafikapo mbele za watoto wao, na utumia fimbo kila wakoseapo watoto wao,
ila kwa jitihada zote hizo bado juhudi zao zinagonga mwamba kwa kutokuwa na
matunda mazuri ya kuwakuza watoto hao, hii ni kwa sababu ukali, fimbo na
makelele mengi havitoshi kumfanya mtoto abadilike, ila kutumia fimbo pamoja na
kumfunza neno la Mungu na likakaa vizuri ndani umfanya mtoto kuwa na hofu ya
Mungu ambayo itamzuia kujishughulisha katika uovu ajishughulishao.
Somo hili linatoa
majibu ya namna gani mtoto anapaswa kukuzwa katika BWANA, na ni kwa namna gani
mzazi anaweza mtengeneza mtoto kuwa katika misingi iliyo myema na ya kupendeza
kwa kufuata misingi ya biblia.
Itaendelea!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni