Wote tunajua maana ya uhuru .Na kama hujui tutasaidiana hapa chini.
Uhuru
ni hali ya kuwa na usismamizi binafsi katika mambo yako.Kama bado huwezi fanya
maamuzi binafsi na kujitawala basi hauko huru.
Tumekuwa
huru katika mambo mengi lakini hili limechelewa sana na limesababisha watu
wengi kutokuendelea.

Nchi
nyingi zilitawaliwa lakini fikra za viongozi mfano Mwalimu Nyerere zililenga
kufanya mageuzi ya kutoka katika utawala
huo kandamizi.
Mtu
anayetawaliwa kifkra huongozwa kama remote katika mambo yake na huwa anategemea
maamuzi ya mtu au watu wengine.
Mtu
huyu hawezi kujisimamia Mwenyewe yaani ni tegemezi na mara nyingi mawazo yako hunyonywa na
wakoloni (ndugu,jamaa na marafiki wenye mitazamo hasi).
Usipokuwa
na uwezo wa kufanya mapinduzi ya kifkra na kutoka mikononi mwa tawala za watu
wenye mitazamo hasi(wakoloni) ni wazi kuwa hautaweza kuendelea katika mambo
yako mpaka unakufa.
Kuna
wakati mwingine nchi zilitumia mtutu wa bunduki ili wawe huru toka vifungo vya
kikoloni Vivyo hivyo unapaswa kufanya kila linalowezekana kujisimamia mwenyewe
kimtazamo/kifkra na kuamua kutofuata mawazo hasi ya watu wasiotaka ufanikiwe
Joas
(Jyb)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni