"Je unafahamu rangi ya Ndizi?
Kuna
siku niliwauliza marafiki zangu
waniambie rangi ya ndizi maana ilinitatiza.Wakataka kujua kama hiyo
ndizi ni ndizi iliyoiva (ripe banana) au Ndizi mbichi .Nikawaambia vyovyote
vile nilitamani kujua rangi ya ndizi.

Walianza kutoa majibu yao kuwa rangi ya ndizi ni kijani kabla haijaiva na njano ikishakuwa imeiva.Aidha niliwapongeza kwa majibu yao mazuri kwa kuwa majibu yao yalitokana na vile walivyoona kwa macho yao na muonekano wa nje wa ndizi(basing to external observation).
Ukweli
ni kwamba Watu wengi hawajui rangi ya ndizi .Rangi ya ndizi ni nyeupe .Maganda
ya ndizi ndo yanaweza kuwa ya rangi tofauti tofauti.Kuna ndizi zingine zikiiva
huwa na rangi nyingine kabisa na siyo rangi ya njano kama wengi wanavyojua
lakini ndizi yenyewe ya ndani ina rangi moja dunia nzima.Kwa hiyo maganda ya
ndizi ndo yana rangi tofauti.
Mfano
huu unatufundisha kuwa Hakuna mtu anayekufahamu vizuri zaidi ya vile
unavyojifahamu.Wanadamu wanakufahamu kwa namna wanavyokuona kwa nje lakini
ulivyo ndani hawawezi kujua .Mwanadamu ana ukomo wake wa kukujua wewe. Hivyo
wewe ndo unayejifahamu vizuri.
Kwa
hiyo vile wanadamu wanavyofikiri upo inaweza kuwa kinyume chake kwa hiyo wewe
ndo unauwezo wa kudhibitisha vinginivyo ili ule uhalisia wako uweze kuonekana
.Uwezo na kila kitu kilichomo ndani yako hakiwezi kuoneka mpaka wewe mwenyewe
uamue kukitoa .Leo amua kuonesha dunia kuwa vile wanavyodhani wewe uko sivyo
ulivyo .
Watu
wengi wanaweza kukudharau kuwa wewe huna chochote kumbe una kipaji ambacho wao
hawakijui na wewe ndo unapaswa kukitoa na kukiweka wazi .Unao uwezo mkubwa
tatizo hujaonesha dunia uwezo ulio nao .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni