“Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Nafsi yake mvivu itaona njaa” ~Mfalme Sulemani
Watu
ambao wamewahi kufanikiwa duniani na wafanikiwao hata sasa ni wale wenye juhudi
katika utendaji wao. Na atendae kwa ulegevu hufa masikini au hufa pasipo
kufikia malengo aliyonayo juu ya maisha yake.
Kinyume
cha bidii ni uvivu, uvivu ni hali ya kuwa mzito kufanya wajibu na mambo ambayo
yanaweza kukuletea maendeleo. Kukosa bidii katika kila jambo na kufanya vitu
sahihi kwa wakati usio sahihi.” Mchungaji John Nengala Lobulu
Uvivu
ni adui mkubwa sana wa mafanikio ya mtu na hutenda kazi kwa kumtia mtu moyo
ndani yake kuwa asijali tu na mara nyingine humtia moyo kuwa wakati wako wa
kupambana bado ukifika mbona nawe utapambana tu. Uvivu unaambatana na hali ya
kupenda usingizi au kupumzika wakati wengine wakiwa katika kufanya kazi.
Mvivu
hapendi kufanya kazi kwa bidii na kutofanya kazi kwa bidii ni kikwazo kikubwa
cha kumfanya mtu asiweze kufanikiwa, na watu wote wafanikiwao katika mambo yote
ni watu wenye bidii ila mwenye mkono mlegevu ni lazima ashindwe kufikia katika
mafanikio makubwa. Uliza mtu yeyote aliyefanikiwa katika mambo yoyote yale
utagundua kuwa ni mtu mwenye juhudi katika utendaji kazi wake kwa kuwa Mungu
anabariki kazi za mikono ya watu wake. Uvivu ndio humfanya mtu ashindwe kufanya
kazi kwa juhudi na husababisha pia watu kutokuziona fursa zilizopo na wavivu
wengi hudharau fursa zipatikanazo kwa kuziona kuwa ni ndogo pasipo kujua kuwa
fursa ndogo hufungua mlango kwa fursa kubwa zaidi.
Uvivu
si katika mambo ya ulimwengu huu tu bali huwa katika mambo ya kiroho pia. Watu
waliofanikiwa katika mambo ya kiroho na kuweza kuwa na mahusiano makubwa na
Mungu ni watu ambao ndani yao hakuna uvivu katika mambo ya kiroho; mtu mwenye
tabia ya uvivu katika roho huwa na hali ya kupuuza maombi yake binafsi na
maombi ya vikundi au kanisa, mvivu wa kusoma na kutafakari neno ambao
husababisha udhaifu katika kutembea katika njia za Mungu na kuwashuhudia
wengine uzuri wa Kristo ili wapate kuokolewa (mvivu kuhubiri injili ambayo ni
agizo kwa kila mmoja), na pia huwa mvivu katika kuhudhuria ibada na ratiba
mbalimbali za kanisa na kufanya mambo mengi ya ujenzi wa ufalme wa Mungu. Uvivu
huu ni dhambi na huleta uangamivu mkuu ndani ya mtu.
Mithali
6:6-11 “Ewe mvivu, mwendee chungu,
Zitafakari njia zake ukapate hekima. 7 Kwa maana yeye hana akida, wala
msimamizi, wala mkuu, 8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;
Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. 9 Ewe mvivu, utalala hata lini?
Utaondoka lini katika usingizi wako? 10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
Bado kukunja mikono upate usingizi. 11 Hivyo umaskini wako huja kama
mnyang’anyi, na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”
Biblia
inautaja uvivu kama kitu kibaya sana na huwa chanzo cha umaskini na hata njaa
kwa mtu mwenye nao, na katika ulimwengu wa roho ni chanzo cha anguko katika
dhambi; na mwenye nao mara zote hujitia moyo kuwa bado kulala kidogo na bado
kusinzia kidogo.
Watu
walio wavivu mara zote hushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea na mara
nyingi malengo hayo huwa katika namna ya hadithi nzuri ila zisizo na hatua
yoyote ya utendaji.
|
Mtu mvivu mara zote hubeba sifa hizi:
·
Hupenda sana usingizi.
·
Hupenda kupumzika hata kama hajafanya kazi.
·
Hujihurumia sana na hupenda sana kuhurumiwa.
·
Hupenda kujitia moyo na kutiwa moyo hata kama amekosea.
·
Hupenda kupokea zaidi ya kutoa na hulalamika sana asipotendewa yeye.
·
Hupenda kulaumu wengine na mazingira yamzungukayo katika makosa yake.
·
Hudharau kazi na hupenda sana kuchagua kazi.
·
Hapendi kuteseka kabisa na ugumu wa shughuli na kuona ni bora kuacha.
·
Hupenda kuvuna asichopanda.
·
Hupenda maisha ya ubwana na kutumikisha wengine.
·
Huridhika upesi kwa kile apatacho.
·
Hajali muda.
·
Hana mpangilio mzuri katika utendaji wa mambo yake.
·
Nyumba yake haiishiwi na uhitaji na njaa.
·
Hana juhudi katika maarifa na kupata ufahamu.
·
Hana juhudi katika kazi/ hana bidii katika ayafanyayo na huvumilia
kazi na si kufurahia kazi.
·
Mzembe katika mambo ayafanyayo.
·
Hakosi sababu ya kujitetea katika jambo lolote akosealo.
Kwa
wanaofanya hesabu ukitaka kupata jibu sahihi ni lazima utumie njia iliyosahihi
ambayo yaweza kuwa njia ndefu au fupi lakini ni njia sahihi na kama utatumia
njia isiyo sahihi ni lazima ukose jibu ambalo unalihitaji kulipata. Ndivyo
ilivyo katika maisha ya kawaida kama unataka kufanikiwa katika njia uiendeayo
ni lazima kuangalia kutenda sawa sawa na njia isemavyo. Kwa maana nyingine ni
kusema hakuna majibu sahihi kwenye matumizi ya njia feki/isiyo sahihi.
Watu
wengi hupenda kupata matokeo ila tatizo ni njia ya kutafuta hayo matokeo
ikikosa usahihi matokeo hayawezekani kuwa sahihi.
Yakobo
4:3 “Hata mwaomba, wala hampati kwa
sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”. Maandiko yanaonyesha
sababu mojawapo ya kutopewa/kutopata ni kwa sababu ya kutokuwa sahihi katika
uombaji au kutumia njia zisizo sahihi. Ukitumia njia yoyote isiyo sahihi ni
lazima matokeo yagome kutokea.
Katika
uhalisia wa maisha chochote unachotaka kukifanya kama ni kwa njia isiyo sahihi
ni ngumu sana kutimia na mwisho wake ni mbaya.
Upande
wa Mungu yeye hawezi kutembea na mtu asiye mwaminifu, na mtu akosaye uaminifu
anajifungia baraka za Mungu yeye mwenyewe katika maisha yake, ila kwa upande wa
sisi wanadamu uaminifu ni sababu kubwa sana ya watu kufanikiwa na kuaminiwa na
hata kupandishwa ngazi/madaraja katika sehemu za kazi au kupendwa na watu zaidi
na hata kama ni mtu anashughuli zake huaminika na kupewa fursa nyingi zaidi.
Mtu asiye mwaminifu si rahisi kabisa kuaminiwa na kukabidhiwa majukumu mengi
zaidi kwa kuwa inaaminika kuwa hawezi hakafanya vizuri na hata kama akifanya
basi utendaji wake unaambatana na ubadhirifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni