UNYOPASWA KUYAFAHAMU KUHUSIANA NA SADAKA YA LIMBUKO
Hii ni sadaka ambayo ni ya mwanzo wa
kila pato ulipatalo katika yale uyafanyayo. Kama ni biashara basi yale mapato
ya kwanza ni malimbuko yako kwa BWANA, kama ni kazi huwa mshahara wa kwanza,
kama ni mazao huwa yale ya kwanza na vivyo hivyo kwa wanyama. Sadaka hii pia
kwa nyakati za leo huwasilishwa kanisani.
Ezekiel 44:30 “Na kitu cha kwanza cha
malimbuko yote ya vitu vyote, na kila toleo la kila kitu cha matoleo yenu, litakuwa la makuhani. Tena mtampa kuhani sehemu ya kwanza ya unga
mbichi, ili kukalisha Baraka juu ya
nyumba yako.
Mithali 3:9:10 “Mheshimu BWANA kwa mali yako. Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. 10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika kwa divai mpya.”
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutoa
malimbuko, na ukweli ni kuwa hii sadaka ni sadaka ambayo haina kipaumbele kwa
watu. Wengi hawafahamu kabisa kuhusu hii sadaka na hata wanaofahamu ni wachache
sana wanaoishiriki ipasavyo.
Ukisoma maandiko hapo juu utaona kuna
Baraka nyingi sana zinatajwa kuambatana na mtu anayetoa malimbuko. Kwenye
kitabu cha Ezekiel anasema Baraka zitakaa juu ya nyumba ya huyo mtu. Kuna
tofauti kubwa ya Baraka kukaa na kuja, zinaweza kuja na kuondoka lakini zikikaa
hudumu mahali hapo hapo bila kuondoka. Maanaake nyuma ya mtu anayetoa malimbuko
si nyumba ya kawaida, ni nyumba iliyojaa Baraka na kila kilichomo ndani yake
kimebarikiwa na kila kizaliwacho ndani ya hiyo nyumba kimebarikiwa pia, na hata
mgeni akiingia kwenye hiyo nyumba ni lazima abarikiwe. Malimbuko yanavuta
Baraka za Mungu kuishi na mtu.
Mtu ambaye kazi yake anaitolea
malimbuko hakuna adui anayeweza kuigusa na kufanya chochote kile anachohitaji
kukifanya. Mtu wa namna hii kuna kuinuliwa ‘promotion’ nyingi zitakuwa
zinafanyika kwa ajili yake.
“kama mazao/mapato yako ya kwanza
yamebarikiwa basi lazima vyote vinavyokuja baada ya hayo view vimebarikiwa”
Watu wengi huwa hawaelewi kuwa sadaka
huwa zinadai Baraka mbele ya madhabau ya Mungu na ndio maana anayetoa sadaka
kwa uaminifu mbele za Mungu maisha yake mara zote siyo maisha ya kawaida.
Dr. Michael Hutton-Wood anaelezea
uzoefu wake katika malimbuko kuwa tangu Mungu amemfunulia siri ya kuelewa nguvu
ya malimbuko akaamua kuinuka na kutembea katika kanuni ya kutii na kutoa. Yeye
kila anapoanza mwaka, mapato yote ya mwezi January lazima ayatoe mbele za
Mungu, na ikiwa mapato yake ya kwanza yamekuwa matakatifu mbele za Mungu basi
mapato yote yatakayokuja baada ya hapo yatakuwa yamebarikiwa.
Napenda kubarikiwa, kumiliki vitu
vizuri kwangu haitoshi, nataka kumiliki vitu vizuri huku nikiwa ndani ya mfumo
wa Baraka za Mungu. Namshukuru Mungu kwa kuifunua siri hii katika maisha yangu.
Ukweli ni kuwa mwezi Januari haswa
kwenye jamii zetu za Kiswahili huwa maarufu kama mwezi mgumu kifedha kwa kuwa
watu wanakuwa wametoka katika msimu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya
lakini pia huwa na majukumu ya kupeleka watoto shule haswa kwa wale wenye
familia, inakuwa ngumu kumwelezea mtu asiyejua maana ya sadaka kuwa anapaswa
kutoa pato lake ili kutakasa mapato yake ya mwaka mzima. Ila sijawahi kumuona
mwenye haki ameachwa kwa sababu ya haki yake.
Hata kama umeangaika kupata kazi muda
mrefu na imetokea umepata halafu unamadeni mengi usikulupuke kuanza kula hela
ya Mungu. Tulia na uipeleke mbele za Mungu (soma tena Ezekiel 44:30),
unapoipeleka mbele za Mungu unasababisha Mungu awe anaiangalia kazi yako kwa
umakini, atailinda kazi yako, hata kama kuna watu wanataka kuipoteza haki yako
ya kufanyiwa promotion hawatakuwa wanapambana nawe bali watakuwa wanapambana na
Mungu mwenyewe na utapewa hata hekima ya kutumia mshahara wako ili isiwe kama
wale walioweka fedha zao katika mifuko iliyotoboka toboka.
Hagai 1:6 “Mmepanda mbegu nyingi
mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na
vinywaji; mnajivika nguo lakini hakuna aonaye moto; na yeye apateye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko
uliotoboka-toboka.”
Bila shaka umeshawahi kukutana na mtu
anakwambia toka aanze kufanya kazi haoni faida yake, hata mshahara anaoupata
haujawahi kufanya kitu chochote cha maana. Siri imejificha humu katika utoaji.
Maana Mungu anasema atamkemea yeye alaye ila kama tukitoa zaka na dhabihu, sasa
atakemewaje yeye alaye kama mtu hatoi?
Mungu anaheshimu sana pale unapoamua
umuheshimu kwa kile ulichonacho na ndio maana kwenye Mithali 3:9-10 anasema
akiheshimiwa kwa malimbuko yetu ni lazima ghala zetu zijazwe kwa wingi na
kufikia viwango vya kufurika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni